Katika teknolojia ya runinga bora, kubwa na za kisasa kampuni ya Sony haiwezi kukosekana kwenye orodha na hii inatokana na utengenezaji wao ambao mara zote umekuwa ukiwafanya wapate kufahamika vyema.
Kwa mara nyingine baada ya miaka mitano Sony wametenegenza runiga kubwa zaidi ya upana wa basi na kutokea kupata mteja mara moja. Mwaka 2014, Sony walitengeneza runinga ya ubora wa 16K na kuiweka kwenye uwanja wa ndege wa Haneda, Tokyo-Japan.
Sasa hii ya mwaka huu wa 2019 ni ya 16K yenye upanda wa mita 19.2 (futi 63) na urefu wa mita 5.4/futi 17 ambapo Sony wametumia teknolojia ya Crystal LED ambapo ndani yake wakaweza kutengeneza mifumo ya LED nyingine ndogondogo inayosaidia kutengenza runingza za ukubwa/ubora wowote ule.

2 Comments
Comments are closed.