Sony wamekuwa wakitoa simu ambazo zimekuwa zikipendwa na watu wengi sehemu nyingi duniani mpaka leo hii ukitamka bidhaa za kampuni hiyo basi mtu hawezi kuacha kuzungumzia mojawapo ya vitu vyao.
Mwishoni mwa mwezi Februari bidhaa nyingi tu za kidijiti zilizinduliwa na makampuni mbalimbali, mojawapo kati ya nyingi zilizozinduliwa nikimaanisha simu janja ilikuwa ni Sony Xperia 1 ambapo simu hiyo inaelezwa kuwa na vitu viwili ambazo havijawahi kuwepo kwenye rununu za Sony zilizopita. Fuatana nami ili uweze kufahamu simu za simu ninayozungumzia kipengele baada ya kipengele.
>Muonekano (Kioo)/Kipuri mama
Kwa mara ya kwanza kabisa Sony wameamua kutumia kioo cha 4K HDR OLED kwenye simu hii. Hii inamaanisha chochote ambacho kinaonekana kwenye uso wa juu kwenye rununu hiyo ni cha ung’avu wa hali ya juu sana. Pia kioo hicho kina urefu wa inchi 6.4, uwiano wa 21:9 (upana wa kioo kama upo sinema). ufanisi wa simu/kifaa cha kidijiti unapewa nguvu sana na aina/uwezo wa kipuri mama; kwenye Sony Xperia 1 ipo Snapdragon 855.
>Kamera
Kwenye upande wa kamera ni kipengele kingine ambacho Sony wameamua kuwa tofauti kabisa na simu zake nyingine zote zilizopita kwani kwa mara ya kwanza simu hiyo ina kamera 3 nyuma, zote zina MP 12 na 2 kati ya hizo zinaruhusu mtu kukuza kitu mara mbili zaidi sawa na 52mm. Kamera ya mbele ina MP 8.

>Memori ya ndani/RAM
Simu nzuri ni pamoja na kuwa na kasi inayowezeshwa na RAM lakini pia uwezo wa kuhifadhi vitu vingi kama memori. Sony Xperia 1 ninayoizungumzia ina GB 6 upande wa RAM, GB 128-diski uhifadhi lakini pia unaweza ukaweka memori ya ziada mpaka GB 512.
>Betri/Mengineyo
Anayemiliki simu janja na mfuatilioaji mzuri wa simu ambazo simu yake inazo basi suala zima la betri huwa analiangalia kwa jicho la ziada. Sony Xperia 1 ina 3330mAh, teknolojia ya kuchaji haraka lakini pia ina teknolojia inayofanya betri liweze kudumu muda mrefu.
Inatumia kadi mbili za simu, mfumo endeshi-Android 9, ina kioo kigumu-Gorilla 6, teknolojia ya kuzuia kuingia maji ipo, Bluetooth 5, USB Type-C, ni simu ya 4G, ina teknolojia ya alma ya kidole, haina redio wala sehemu ya kuchomeka spika za masikioni.