Naaaam, mauzo ni makubwa sana sio? Vipi katika upande wa faida sasa? Ni wazi kuwa Sony kupitia PlayStation ni moja kati ya makampuni makubwa sana katika maswala ya magemu.

Japokuwa kampuni tayari imeshauza PlayStation hizo zipatazo milioni 25 lakini bado kampuni inatarajia kuendelea kuuza nakala zingine milioni 18 mpaka mwaka huu kuisha.
Mauzo haya yamewekwa wazi kwenye repoti ambayo imetoka katika mwaka wa fedha unaioshia septemba 30, mwaka 2022 na mauzo hayo yanajumuisha yale yote –ya PlayStation 5– yaliyofnayika duniani kote.

Ukaichana na ukuaji wa mauzo wa kampuni lakini bado Sony wanasema wanapata faida ndogo sana na hii ni ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Kwa sasa wanasema gharama kama vile za uendeshaji na uzalishaji wa magemu umekua sana, na ukaichana na hayo bado kuna gharama nyingi sana zinazoenda kutokana na mchakato mzima wa kununua makampuni mengine kama vile walivyoinunua Bungie.

Kwa mwaka wa fedha unaoishia machi 2022 kampuni ya Sony ilitangaza kuwa iliuza PlayStation 5 milioni 11.5 na kushindwa kufikia matarajio ya milioni 14.8 ambayo walikua wamejiwekea.
Hii ilikua ni kwa sababu ya kutopatikana kwa wakati (upungufu) kwa baadhi ya vipuri ambavyo vinatumika katika kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinatengenezwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hii umeipokeaje? Unadhani kampuni itaweza kuendana na kasi na kuuza hizo nakala milioni 18 mpaka mwaka wake kuisha?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.