Kwa mara ya nne Space x wamefanikiwa kutua roketi katika meli baada ya kuitumia kupeleka mzigo katika anga.
Jambo hili lilikuwa ni ndoto miaka kadhaa iliyopita na kufanikiwa kwake ni dalili kwamba sasa roketi zitatumiwa kwa zaidi ya safari moja jambo ambalo litapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kurusha roketi angani jambo ambalo litasaidia uvumbuzi katika anga kufanyika kwa kasi zaidi.
Safari hii Falcon 9 ilikuwa imebeba setelaiti ya mawasiliano ya nchi ya Thailand iliyopewa jina la Thaicom ambayo ni setelaiti ya kibiashara. Changamoto kubwa ambayo ilikuwa inawakabili Space X ni kwamba roketi hii ilikuwa kutokana na umbali ambao roketi hii ilikuwa inaenda (Roketi ambazo zinapeleka setelait kwaajiri ya kuzunguka dunia huwa zinakwenda umbali mrefu zaidi ya zile zinazopeleka mizigo katika kituo cha kimataifa cha anga ISS) kulikuwa na wasiwasi kwamba ingeshindwa kufanikiwa kurudi bila matatizo makubwa katika uso wa dunia.

Kwa lugha nyepesi unapotaka kupeleka mzigo katika anga (Tuchukulie mfano Setelaiti) unahitaji kuipakiza katika Roketi kisha kuirusha hiyo roketi na pindi itakapofika katika kimo ambacho unataka huo mzigo wako ukae (Hii hutegemea na matumizi ya kifaa ulicho rusha) roketi huuachia mzigo ambao kwa kutumia injini zake utaanza kuelea na kufanya kazi yake.
Roketi kwa upande wake hushuka na kurudi duniani ambapo tangu sayansi ya anga ilipoanza roketi zimekuwa zinarudi duniani kwa kuanguka baharini na ni vigumu kuzitumia tena baada ya zoezi hili. Space X walikuja na wazo la kuhakisha kwamba kila roketi inayopeleka mzigo angani basi haitupwi baharini baada ya kufikisha mzigo ila narudi duniani na kutua kisha inatumiwa tena na tena ili kupunguza gharama za uendeshaji.
Roketi hii ilikuwa inakimbia kwa mwendo wa kilomita 6300 kwa saa ilipokuwa inaingia katika anga ladunia na iliweza kupunguza mwendo mpaka kilomita 4 kwa saa wakati inagusa meli maalumu iliyowekwa kwaajiri ya roketi hiyo kutua. Mafanikio haya yanaonesha kwamba kutua kwa roketi ikiwa inaenda kwa mwendo mkali inawezekana.

Hii ni mara ya nne Space X wanatua roketi kwaajiri ya kuitumia tena baadaye na ni mara ya tatu inafanyika katika meli maalumu baharini.
Soma Pia
- Space X yashindwa jaribio la kutua roketi katika meli
- Space X yafanikiwa kutua roketi katika meli.
Makazi binafsi kuja katika anga. - Majaribio ya makazi ya Kujazwa upepo ya kwama
Makala hii imeandikwa kwa msaada wa makala mbalimbali zilizochapishwa mitandaoni juu ya tukio hilo kama vile The Telegraph
One Comment
Comments are closed.