Wengi walidhani ingekuwa ni jambo gumu kwa Space X kuweza kupata wateja wa kuwapeleka kwenye mwezi si kwa ajili ya utafiti bali kwa matembezi tu na kuweza kujionea yaliyoko huko mwezini.
Safari hiyo ambayo wakati inatambulishwa rasmi kwa ulimwengu karibu mwaka mmoja uliopita ilisema kuwa kwa mtu atayetaka kwenda kwenye mwezi mtagharimu dola za kimarekani takribani bilioni 10 sawa na 220Trn kwa pesa za Tanzania.
Watu hao wawili na wengineo (kama idadi ikiongezeka) wanatarajia kupelekwa huko kwenye mwezi mwaka 2018 ambao tayari wameshafanya malipo kwa kiasi fulani cha kuridhisha kwenda kwenye akaunti ya Space X, kampuni binafsi inayomilikiwa na Elon Musk.
Ingawa kiasi kamili walicholipa wateja hao wala majina yao havijawekwa wazi ila itakuwa ni mara ya kwanza kwa binadamu kusafiri umbali zaidi kuzidi Orbit ndogo ya sayari yetu (Dunia).
Machache kuhusu Space X
- Space X wanasifika zaidi kwa kupelekwa vyombo (roketi) vyao angani na kisha kurudi salama hivyo kuweza kutumika tena kwa mara nyingine pale inapohitajika.
- Shirika hilo lina mahusiano ya karibu na shirika la Marekani linalojidhughulisha na masuala ya anga yaani NASA. Ushirika huo unathibitika kwa Space X kuhusika katika uundaji wa roketi na Dira kwenda NASA.
- Space X ndio shirika la kwanza kupeleka roketi angani na kruudi chombo hicho kikiwa salama ingawa ni baada ya majaribio kadhaa-SPACE X Yashindwa Jaribio lake la Kutua Roketi katika Meli (hakuna mwanasayansi aliyefanikiwa mara moja tu baada ya kufanya jaribio).

Kifaa chicho ambacho kitakuwa katika mfumo wa ‘automatic‘ ambapo hapatakuwa na watu wengine isipokuwa tu watu wao watakao kwenda huko mwezini ingawa wafafundishwa jinsi ya kujiokoa iwapo chombo hicho kitapata hitilafu ya aina yoyote ile.
Mafanikio ya Safari hiyo yataendelea kuimarisha Space X katika masuala ya anga na kupigilia msumari wa uaminifu kwa walio wengi ambao si mabalozi wazuri wa Space X kutokana kutoamini ambacho kinafanya.
Vyanzo: Npr, mitandao mbalimbali
One Comment
Comments are closed.