SpaceX na jaribio jingine la Starship, nalo limeenda vizuri hatua zote ila likaenda vibaya tena kwenye kutua. mashabiki wa makubwa yanayofanyika katika sekta ya teknolojia za anga, kama mimi 😀 tarehe 2 Februari wote tulikuwa tunasubiria kwa hamu na kutazama majaribio mengine ya teknolojia za ndege ya Starship.
Haya ni majaribio ambayo yashahairishwa mara kadhaa kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi – ila kutokana na hasira za Bwana Elon Musk na vyanzo vingine inaonesha shirika la kusimamia safari za anga la Marekani, FAA, ndio lililosababisha uchelewaji wa majaribio haya kwa siku kadhaa sasa.
Lengo la majaribio
Kupitia SN9 kampuni ya SpaceX inajaribu kupata data za maboresho juu ya utengenezaji wao wa ndege inayotakiwa kuweza kufanikisha safari kati ya dunia yetu na sayari ya Mars, lakini pia ndege hiyo hiyo kuweza kufanikisha safari za duniani kwa miji miwili iliyo mbali ambayo kwa sasa safari zinachukua zaidi masaa matano au nane, na kufanya safari hizo kufanyika chini ya lisaa limoja.
Kupitia Starship, kampuni ya SpaceX itaweza kufanikisha safari za miji ya mbali duniani ndani ya muda mchache, lakini pia ni lengo la SpaceX kutumia teknolojia hii kuwezesha safari za kwenda kutoka duniani kwenda kwenye sayari nyingine.
Majaribio yameenda vibaya, tatizo nini?
Katika majaribio haya, kwa mara nyingine tena ndege hiyo imeshindwa kurudi na kutua salama. Kwa sasa wataalamu wengi walioangalia video ya kutua wanaona kutakuwa na tatizo limefanyika katika kompyuta ya rokeni hiyo – roketi ilishindwa kujiweka kwenye wima unaofaa na pia ikawa imeshashuka chini sana.
Injinia mkuu wa SpaceX Bwana John Insprucker amesema “Kwa mara nyingine, ndege ilikuwa na safari nzuri…. inabidi tuongeze kazi katika kuboresha utuaji”.
No Comment! Be the first one.