Spotify inajihusisha moja kwa moja na App ya HealthKit ambayo inapatikana katika vifaa vya iOS, dhumuni likiwa ni kuandaa miziki kulingana na taarifa zako za kiafya zinazopatikana kupitia HealthKit.
Spotify ni mtandao ambao unatoa huduma ya muziki wa Ku’stream, na kwa sasa imeripotiwa kuwa iko mbioni kuja na kipengele hicho lakini inaonekana dhahiri pengine hii inaweza ikawa katika vifaa vya Apple tuu.
Hapa kinachoonekana ni kwamba Spotify inachagua au kushauri baadhi ya nyimbo ambazo zinaendana kabisa na taarifa zako za afya ambazo zipo katika App ya HealthKit.
Kinachofanyika ni kwamba huduma zote mbili zitaingiliana na dhumuni lenyewe ni kuhakikisha kuwa mtumiaji anapata kitu kizuri zaidi.
Ni wazi kwa sasa huduma ya Spotify inakua inatoa hudama ya muziki wa orodha (Playlist) ambayo unaweza ukaanda mwenyewe au vile vile hata mtandao unaweza ukawa unashauri orodha.
HealthKit integration in Spotify under development. https://t.co/f1FwRWzzoi pic.twitter.com/BIrydscOV1
— @chrismessina@mastodon.xyz (@chrismessina) December 21, 2022
kingine watu wanachohoji ni kwamba huduma hii waifanye mpaka ifike kwa vifaa vingine kama vile vifaa vya Android n.k
Fikiria huduma hii ikivuka zaidi na kuanza kupatikana kwingine ukiachana na iOS tuu, jambo hili litakua ni zuri maana watu kupitia vifaa tofauti tofauti watakaua na uwezo wa kupata huduma hii.
Kingine cha kujua mitandao kama Spotify, Youtube na mingine mingi huwa ina tabia ya kufuatilia kwa ukaribu vitu unavyopenda kuviangalia na kuvisikiliza na kisha kukuletea tena vitu vinavyofanana na hivyo
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani huduma hii itakuja na kusogea katika vifaa vingine kama Android na vingine vingi kama simu na saa janja mbalimbali kutoka makampuni tofauti tofauti.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.