Ndio kipengele cha ‘community’ kinakuja katika App ya Spotify, kazi kubwa ya kipengele hichi ni kwamba hapa utakuwa na uwezo mkubwa wa kujua mienendo ya marafiki zako .n.k
Ukaichana na hili mtandao wa Spotify kwa kipindi cha muda mrefu imeakua ikiweka vipengele ambavyo mara kwa mara vimekua ni vya kijamii Zaidi
Mfano mkubwa ni uwezo wa watu kushirikishana (share) kwa nyimbo au kundi la nyimbo wanazosikiliza kupitia mitandao ya kijamii na pia hata kujua rafiki yako anasikiliza nyimbo gani (za aina gani).
Kwa haraka haraka ni kwamba Spotify ya mtandao ilikua ina vipengele vingi sana vinavyohusiana na marafiki kuliko ile ya Android na iOS, hili litabadilika sio?
Huduma ya ‘community’ itabadilisha mambo mengi sana katika App japokua kwa sasa huduma hii ndio ipo katika hatua za maandalizi.
Kwa haraka haraka ni kwamba hapa —katika kipengele cha community — utakuwa na uwanja mkubwa sana wa kuweza kuona mambo mengi kuhusiana na marafiki zako.
Mfano ni nyimbo gani wamekua wakisikiliza hivi karibuni, vitu gani wana’stream?, vile vile utataarifiwa ni kitu gani wanasikiliza kwa wakati huo n.k.
Bado haijawekwa wazi kuwa ni lini Spotify itaachia kipengele hichi kwa hadhira yote, lakini hatuna bidi kusubiri
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini kwenye uwanja wa comment, je unadhani kipengele hichi kitaboresha matumizi katika mtandao huo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.