Spotify ni jukwaa kubwa sana la muziki tena ule wa kustrem, licha ya kuwa moja katika ya jukwaa maarufu sana kuhusiana na mzuiki.
Pia Spotify ni moja kati ya mitandao ya muziki ambayo inawalipa vizuri sana waandaaji wake wa maudhui, licha ya hivyo bado waandaaji hao wamependelewa kwa kuletewe kipengele kingine kipya.
Spotify ilichofanya hapa ni kuongeza kipengele ambacho kitawasaidia hata hao wasanii waweze kuuza bidhaa zao kwa urahisi.
Ni wazi kwamba wasanii wengi huwa wanaimba muziki lakini kupitia chapa (brand) zao huwa wanakua na biashara zingine za pembeni kama vile kuuza nguo ambazo zina nembo zao.
Kinachofanyika hapa ni kwamba kipengele hichi kitoanyesha bidhaa zote za msanii huyo katika eneo moja na kwa urahisi kabisa.
Kipengele hiki kina jina kabisa na kimewekwa peke yake katika mtandao huo na kinaitwa ‘Merch’ ambapo ukiingia hapo kila bidhaa ya msanii husikia utaipata hapo.
Ni kawaida kwa mtandao wa Spotify kuleta matoleo mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanawavutia watumiaji wengi Zaidi huku wakihakikisha wale waliobakia wanabakia
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani kwa njia hii kampuni itapata watumiaji wengi Zaidi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.