Kama unapenda kusikiliza muziki mtandaoni na ni mkereketwa wa teknolojia bila shaka utakuwa unafahamu huduma ambayo Spotify wanatoa kupitia intaneti.
Kampuni hiyo (Spotify) wameamua kutoa app mpya kabisa kwa ajili ya saa janja za Apple ambapo wahusika wameweka huko ili kuwavutia watumiaji kulingana na sifa ilizonazo:
Uwezo wa kuunganisha programu tunishi husika na spika au kifaa cha kidijiti. Imeelezwa kuwa programu hiyo inahusiha maboresho wa jinsi muziki unavyotoka hivyo kufanya mtu kupata ladha ladha inayovutia kwa kile anachosikiliza.
Uwezo wa kucheza kitu kilichoshuwa kutoka mtandaoni (Podcast). Mbali na kuwa na uezo wa kucheza muziki kupitia mtandaoni pia programu tumishi husika inao uwezo wa kucheza miziki/picha jongefu zilizoshushwa kutoka mtandaoni.

Uwezo wa kusikiliza musiki bila kutumia intaneti. Programu tumishi mpya ya Spotify imeahidi kuboreshwa kwa toleo litakalofuata mabapo mtumiaji ataweza kupata huduma bila ya kuwa hewani, yaani kuunganisha intaneti ili mtu aweze kupata kile ambacho programu inaweza kufanya.
Ili kupata programu tumishi husika ni lazima uwe unatumia Spotify (v.8.4.79) uliyoshusha kutoka kwenye soko la programu tumishi (Apple Store).
Vyanzo: Tech Crunch, The Verge