Kampuni ya Statoil wikii hii imefanikiwa kupata kibali cha kujenga mradi mkubwa zaidi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia tabaini zinazoelea kutoka kwa selikari ya Scotland ambako ndiko mradi huu utafanyika.
Kibali hiki kitawaruhusu Statoil kusimika tabaini tano zinazofua umeme kwa kusukumwa na upepo, tabaini hizi tano kila moja inauwezo wa kuzalisha walau Megawati sita na hivyo mradi huu utakuwa na uwezo kuzalisha megawati 30.
Mradi huu ni wa aina yake kwani ndio utakuwa cha kwanza kuwa na tabaini zinazoendeshwa na upepo (nyingi sehemu moja) na zinazoelea, Ieleweke wazi kwamba njia nyingine za kuzalisha umeme kwa njia ya tabaini zinazoendeshwa na upepo zimekuwa zikitekelezwa katika maeneo ya nchi kavu.
Mradi huu ambao umekuwa kuwa kikibuniwa na kufanyiwa tafiti kwa muda mrefu utatekelezwa pwani ya mbali kidogo ambako upepo ni wa kutosha kwa kipindi kirefu, pia kwa kuwekwa mbali na fukwe kutaruhusu shughuri mbalimbali kuendelea katika fukwe bila ya bughuza yeyote. Mradi huu utaondoa kero zilizokuwa zinaletwa na mitambo ya kufua umeme kwa nguvu za upepo ikiwamo ile maarufu kwa uchafuzi wa vivutio vya utalii kwa kuzuia watu kuona madhari nzuri.
Miradi kama hii inayafaa mataifa ambayo yanapakana na bahari kama ilivyo kwa taifa letu la Tanzania, mradi huu tofauti na ule unaotumia mabwawa ya maji kama Mtera na Kidatu hautafika wakati kuhitaji kuzima kabisa mitambo kwa sababu upepo hamna maana upepo wa baharini sio wa msimu kama ilivyo maji ya mito. Pia mradi huu unatumia upepo ambao tofauti na gesi ukitumika kuzungusha tabaini hauishi bali unaendelea kuwepo.
Tunategemea kuwa Statoil itafanikiwa kutekeleza mradi huu na hivyo kuikuza teknolojia hii ili ije itumike katika nchi zinazoendelea kama Tanzania ambazo moja ya changamoto zetu ni upatikanaji wa nishati hii muhimu ya umeme kwa uhakika na bei inayoridhisha. Lakini hii pia iwe ni changamoto kwa wanasayansi na watunga sera wetu kujaribu kutafuta vyanzo vya nishati mbadala ili tuweze kusonga mbele.
One Comment