
Tablet- ni jamii ya vifaa vya kompyuta vyenye muundo mdogowa kuweza kubebeka na kutumika mkononi.NI rahisi sana kuziona kama simu, ila tablet imeangukia katikati yasifa za simu na laptop/au compyuta za mezani.Ila wakati simu zinatengenezwa kwa ajili ya masaliano yakupiginiana simu, meseji na matumizi madogo ya intanetiTablets zimejikita katika kukuletea uwezo unaofana na kompyuta za kawaidakatika kutumia intaneti, kufanya kazi zingine kwa urahisi zaidi na pia kwa ajiliya matumizi kama ya kuangalia filamu.Pia kwa tablet unaweza fanya kazi zako kiurahisi sana ambazo vingenevyoungefanyia kwenye kompyuta, ila kama upo safarini,au mazingira yasiyo poa sana basi tablet ni faida kwa sababu ya udogo wake na uwezo wa betri kuhifadhi umeme kwa muda mrefu kulinganisha na laptops.
Je, kwa nini watu wengi wanaziita IPad hapa kwetu? hii ni kwa sababu wengi wanaijua tablet iliyoletwa na kampuni ya Apple, watengenezaji wa simu za IPhone. Kwa ujue ya kuwa IPad ni jamii ya tablet, na kwenye soko la tablet zipo nyingine nyingi kutoka makampuni mengine mengi kama Samsung, Sony, Lenovo na mengine mengi. Na kwa sasa Microsoft!!!!!
Jijini Los Angeles Microsoft watangaza ujio wa Surface
Tablet hii inayotegemewa kuingizwa sokoni mwishoni wa mwaka huu itakuja na mwonekano mpya wa sura wa Windows 8 ujulikao kama ‘Metro’. (Ukitaka kujua zaidi kuhusu Windows 8 tembelea makala ‘Kaa Tayari Kwa Windows 8’ hapa)
Watu wengi wanauona ujio huu ni kushindana na kampuni ya Apple watengenezaji wa IPad, pamoja na Samsung, na makampuni zingine ambao wao pia wanatengeza tablets aina ya Android.
Surface;
Kuanzia muonekano wake inavutia, inakioo cha ukubwa wa inchi 10.6 na kibodi (keyboard) unayoweza kushikiliwa na nguvu za magineti kwenye eneo la chini la tablet hiyo. Hii ni moja ya utofauti sana, kwani kwa kifupi Microsoft wanataka kukufanya usahau laptop au kompyuta yako ya mezani kabisa!
Itatoka na toleo mbili tofauti, kutakuwa na Surface, yenye Windows RT (ambayo inamtazamo wa Metro tuu) na Surface Pro itakayokuwa na Windows 8 pro.
Tofauti kubwa ni hilo suala la Metro katika surface huwezi kulitoa, yaani utakuwa na mtazamo huo mopya tuu. Wakati katika Surface Pro utaweza kuamua kutoka kwenye muonekano wa Metro na kutumia muonekano unaofanana kidogo na huu uliozoeleka katika Windows 7.
Surface, zitakuwa na diski ya ukubwa wa GB 32 na 64, wakati Surface Pro zitakuwa za aina mbili, zenye GB 64 na 128. Hizi tablets zitakuwa na sehemu ya kusoma kadi za kamera, na USB 3. Surface zitakuwa na uzito wa rakribani kilo 0.7 wakati Surface pro zitakuwa na takribani uzito wa kilo moja.

Hadi sasa ndo hivyo, kwa kifupi tunaweza sema waliamua kututaarifu mapema ili tujue kuna kitu kipya kinakuja, lakini vingine vingi wamesema wataviongelea baadae! Kwani ata bei haijulikani zitauzwaje, lakini watafiti wengi wanaona itakuwa kati ya dola 500 hadi 1000, lakini ikitaka kuleta ushindani wa kweli itabidi washushe zaidi.
Na pia imeleta mchanganyiko kwa watengezaji wa tablets ambao nao wanategemea kutengeza tablets zitakazotumia Windows 8, yaani kampuni kama Samsung, Asus, Acers na wengine wengi. Kwa wao inawabidi kuwa ingia gharama ya zaidi ya dola 80 kwa kutumia Operating System ya Windows kwa kila kifaa, hivyo vifikiria na sasa wanashindana na mtu anayewapatia operating system. Watafiti wengi wanaliona hili pia kama litaleta matatizo zaidi kwa Microsoft kwani makampuni haya yanaweza yakazidisha kutoa zinazotumia system za Android (Google) na Ubuntu ambazo wanapatiwa kuzitumia bure kwani ni familia ya Linux operating system.
Ni hayo tuu….unaonaje? Kama unaitamani nunua kibobo kabisa, kwa angalau laki kwa mwezi jua hadi mwakani januari utaweza miliki Surface ikiwa bado ya motoooo!!!! hahahahhaha!!!!
No Comment! Be the first one.