Swiftkey ni moja kati ya keyboard za mbadala ambazo unaweza kuzipata katika mtandao, kwa kawaida keyboard za aina hii zinakua zina vitu vingi vya nyongeza ukilinganisha na ile ya kawaida.
Kuna muda tuliandika kuhusiana na Microsoft ambao ndio wamiliki wa App hiyo ya swiftkey, wamiliki hao walitangaza kuwa wataiondoa App hiyo katika soko la App la App, App Store. Soma Zaidi >>HAPA<<
Microsfot wakati wanasema wana mpango wa kuachana na App hiyo vile vile hawakutoa sababu juu ya kwanini wamefanya maamuzi hayo na hiki ni moja kati ya kitu ambacho watu walijiuliza sana.
Japokua mpaka zaoezi zima la kutangazwa kufutwa kwa App hiyo halikua la kushangaza kwasababu viashiria vingi vilikua vinaonekana wazi wazi mfano kutotolewa kwa sasisho (update) muda mrefu.
Taarifa ambayo iliyoka kama ya App hiyo kufutwa ni kwamba hata kama ikifutwa katika soko lakini ukiwa nayo katika simu yako ya iPhone basi utaendelea kuitumia kama kawaida lakini ndio hutaweza kupata mambo mapya katika app hiyo kama vile masasisho.
Kingine kizuri ni kwamba App hiyo kwa sasa imerudishwa katika soko la App Store na itaendelea kutumika kama kawaida katika vifaa vya iOS.
Microsoft SwiftKey Keyboard is BACK on iOS! 🎉🎊🍾🥳
Stay tuned to what the team has in store for it!
Link ➡️ https://t.co/X6eIq0VJgP pic.twitter.com/23OA67UynZ
— Vishnu.one (@VishnuNath) November 18, 2022
Kwa sasa unaweza ukaipata App ya SwiftKey katika iOS kwa kuingia katika App Store, na kwa wale wa Android wanaweza kupata katika version is available Play Store na katika masoko haya yote inapatikana bure kabisa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unaona ni sawa kwa Microsoft kuifufua App kwa watumiaji wa iOS?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.