Kampuni ya Microsoft watoa taarifa kuwa vifaa vitakavyokuwa vinatumia Windows mpya ya 8 vitakuwa madukani kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu.
Hayo yalisemwa katika Mkutano wa Microsoft Worldwide Partner, Microsoft iliwaambia washirika wa kampuni hiyo (kampuni zinazotengeza kompyuta) inatarajia kutoa Windows 8 RTM mapema Agosti.
RTM inasimama kwa ajili ya ‘Release To Manufacturing’ hivyo hii inamaanisha Microsoft inaweza ikawa katika hatua za mwisho wa kujenga Windows 8 tayari kutuma kwa watengenezaji wa kompyuta na wadau wengine haraka mwezi ujao ili waweze kukamilisha maandalizi ya miundo kwa ajili ya kompyuta ambazo zitaingizwa sokoni na mfumo wa Windows 8 baadaye mwaka huu.
Kwa habari kuhusu bei na mambo mengine yahusiyo Windows 8 angalia katika makala zetu zilizopita!
No Comment! Be the first one.