Tuna mitandao ya kijamii mingi sio? ngoja leo tulenge Facebook maana wengi tupo huko na ndio mtandao unaoongoza kuwa na watu wengi. Sasa basi hivi unajua kama katika Facebook(akaunti yako) kuna baadhi ya marafiki ambao ni ‘feki’.?
Marafiki wa Facebook – Feki ikimaanisha mahusiano yenu katika mtandao huo hayastahili kupata sifa ya ‘urafiki’…miezi na ata miaka mtu yupo na hamjawahi kuwasiliana…..bado ni rafiki huyu?
Kutokana na tafiti iliyofanyika imegundua kuwa baadhi ya marafiki zako ndani ya mtandao huo wa Facebook ni ‘feki’. Yaaani ni wale marafiki ambao hawakujali na hata hawakuonei huruma na matatizo yako hata kidogo. Watu hawawezi wakawa na marafiki wa ukweli juu ya 200 katika mtandao wa Facebook kwa kuwa kunakuwa na mipaka katika kutengeneza urafiki na kuwasiliana
Katika marafiki wa Facebook 100+ unaweza wategemea wanne tuu!
Utafiti huu uliofanywa na Bw. Robin Dunbar ambaye ni profesa wa saikolojia katika chuo kikuu cha Oxfrod, watu wana mamia ya marafiki lakini cha kushangaza ni kwamba katika wastani wanne tuu ndio watakua wanategemewa (kati ya hao mamia).
Bw. Robin Dunbar amesema kuwa alifanya tafiti hii makusudi ili kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya rafiki wa kimtandao na rafiki ambe hayupo katika mtandao ambao unaweza ongea nae kila siku kwa mda wote unapomuhitaji.

Katika utafiti huo, kwa wastani mtu alikua na marafiki 150 na kati ya hao kulikuwa na 14 tuu ambao walikuwa wakijali na kutoa ushauri juu ya matatizo fulani fulani na pia hata kuona huruma. Wastani wa watu waliohusishwa katika utafiti huo wamesema kuwa kwa wao wanafikiri kuwa asilimia 28 tuu ya marafiki zao wa facebook ndio wa ukweli.
Lakini kumbuka hakuna mtandao wa kijamii wowote ambao uaweza kuzuia marafiki wa karibu kuwa ‘watu wanaojuana tuu’ kama marafiki hao hawatakua na muda wa kukutana uso kwa uso mara kwa mara. Kuonana mara kwa mara ni njia nzuri sana ya kudumisha urafiki baina ya watu .
Pia mitandao ya kijamii inaweza kuzuia kuvinjika kwa mahusiano, kumbuka wawili wanaweza kuwa mbali lakini kwa kutumia mitandao ya kijamii wanaweza ongea hata kama hawapo uso kwa uso.
Tafiti inasema kuwa urafiki wa dhati unahitaji muda wa kukutana na huyo mtu unaemuita rafiki mara kwa mara ili kuimarisha urafiki huo.
Tafiti hii iliyofanywa na Bw. Dunbar ilikuwa kwa lengo la kupima kuwa kutumia au kutotumia facebook je, kunawawezesha watu kupata marafiki?
No Comment! Be the first one.