Password meters zina udhaifu kwa kutofanya kazi vyema, hii iwe tahadhari kwa yule mwenye mpango wa kujiunga na mtandao wowote.
Unapojiunga katika mtandao/tovuti fulani na kufikia katika ya kuweka nywila na hivyo kuhakikiwa, kazi hiyo hufanywa na Password meters. Kwa tafiti za zilizowahi kufanyika zilibani password meters kushindwa kutambua kama nywila (nenosiri) uliyoiandika kama itakuwa na ulizi wa kutosha au la!

Pale nenosiri uliyoweka inapokataliwa huwa inaweka alama nyekundu na pale unaweka nywila sahihi basi sehemu ile ya nenosiri huwa inabadilika na kuwa ya kijani.

Ni tumaini la kila mtu kwamba password meters zinafanya kazi ya uhakiki iwapo nenosiri ulloweka itakuwa salama lakini kwa upande mwingine wa shilingi vifaa hivyo havifanyi kazi hizo kwa usahihi.
Njia sahihi ya kufanya jaribio la kutaka kujua iwapo nywilwa yako ipo salama ni kwa kujaribu kudukua akaunti yako na kazi hiyo itahitaji utaalamu kudukua.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa nyilwa unayoichagua iwe na mchanganyiko wa herufi, namba na alama mbalimbali kwa mfano ‘M@tG3rTh1mAn‘ ili kufanya akaunti yako iwe ni vigumu kudukuliwa. BOFYA HAPA kujua namna ya kutengenza nenosiri gumu.
Je, ulitengeneza nyilwa imara sana na kufanya iwe ni vigumu kwa akaunti yako kudukuliwa? Tuambie maoni yako katika sehemu ya comment hapo chini. TeknoKona ipo na wewe kiteknolojia zaidi.
Vyanzo: The guardian, the register