Umekwisha nunua memori kadi (SD Card) ya GB 4, 8 n.k kisha muda wa kuitumia unagundua ni nusu ya ujazo huo uliokua umeandikwa kwenye kadi? Au data zinakuwa zinapotea mara kwa mara…Basi ujue umenunua SD Card feki.
Wengi huwa wanajikuta wanatumia pesa zaidi wakijua wanapata memori kadi ya ukubwa unaoonekana juu ya kadi hizo lakini mwisho wa siku ni utapeli tuu.
Tunashukuru walioulizia juu ya jambo hili na leo tutakufundisha njia kadhaa za kuzitambua kama ni orijino au feki.
> KABLA YA KUNUNUA
Fahamu aina za Memori kadi (SD Card)
Kuna aina kuu tatu. Hapa cha muhimu kujua ni kuzifahamu hizi alama zake, ukikuta memori kadi imeandikwa ina ukubwa wa GB 8 na huku ukiiangalia haina alama ya familia hiyo basi utambue unanunua kimeo.
Aina |
Ujazo |
SDSC or SD |
Hizi zina ukubwa wa hadi GB 4 |
SDHC |
Ukubwa wa GB 4 – GB 32 |
SDXC |
Ukubwa wa GB 64 – TB 2 |
Fahamu tofauti za muonekano wa logo na majina yake, SDSC(SD), SDHC na SDXC…pia kiasi cha ukubwa unaotegemewa kwa aina hiyo ya memori kadi. Ukiona tu haviendani ujue unanunua bomu. Kuna viwanda vingi bubu vinavyotengeneza memori kadi na kuiga majina ya makampuni makubwa lakini huwa hizo logo wanaweka ovyo ovyo tuu.
>USHANUNUA NA HAUNA UHAKIKA
Kama umeshainunua na unaona inasumbua sumbua na unataka kujipa uhakikisho wa ubora wake basi fuata njia hizi. Moja ya kwenye kompyuta na nyingine ya kwenye simu.
Kwenye Kompyuta
Kuhakikisha kwenye kompyuta kuna programu kadhaa, leo nitazitaja mbili zaidi zinazoaminika.
Kuna H2testw na FakeFlashTest. Kupitia programu hizi utaweza kufahamu ujazo wa ukweli ulio kwenye memori kadi au ata USB Flash. Hakikisha unazi’test’ mpya mara baada ya kununua ili kujihakikishia na hivyo kuwahi kurudisha kama inawezekana. H2testw ndio maarufu zaidi.
Download
Kwenye Simu
Pakua app moja inaitwa SD Insights.
Weka memori kadi yako kwenye simu na fungua app ya SD Insights. Inatakiwa kukupa taarifa zote muhimu kuhusu memori kadi yako.
Kama ni orijino au feki basi utapata kujua. Utapata taarifa sahihi za ujazo (storage) wake, kampuni iliyoitengeneza, tarehe ya kutengenezwa na kama ni kimeo utafahamu pia.
Download
Muhimu kujua: Ni kawaida memori kadi ya ukubwa flani, mfano GB 4, kuwa na kama GB 3.8 hivi badala ya 4 kamili. Tunachoongelea hapa ni tofauti kubwa.