Mtandao wa WhatsApp kwa muda sasa umekua ukiwashangaza wengi maana uko tofauti na mitandao mingine ambayo inamilikiwa na kampuni la Meta.
Mitandao mingine yote ambayo inamilikiwa na kampuni la Meta yote ina huduma za matangazo lakini WhatsApp pekee imeonekana ikiwa tofauti.
Hili linaenda kubadilika hivi karibuni na kampuni imekiri jambo hilo linakuja katika mtandao huo maarufu wa kijamii.
Hapa wengi wanajiuliza je matangazo hayo yatakaa katika kipengele gani cha mtandao huo, jibu ni kwamba kuna maeneo mengi ambapo mtandao huo unaweza kuweka matangazo mbalimbali.
Kwa kuanzia tuu WhatsApp wataanza na matangazo hayo katika maeneo ya Channels (kipengele ni kipya / hakina mud asana) na katika upande wa Status.
Kumbuka tayari kuna WhatsApp Business kwa ajili ya wafanya biashara, hii inaonyesha dhahiri kwamba kipengele hiki kitawasaidia sana katika kuvuta wateja katika biashara zao.
Lakini hapo hapo linakuja swali, je vipi kwa wale watu ambao huwa hawapendi kuona matangazo, je watalipia zaidi huduma hii ya WhatsApp ilimradi wasikutane na matangazo?
Hii inaweza ikawa ni njia nyingine kwa WhatsApp kuweza kukusanya mapato ukiachana na kutegemea matangazo hayo tuu.
Kwa haraka haraka hakuna kitu kitawakasirisha wengi kama matangazo yakitokea katikati ya mazungumzo ya watu — sehemu zingine zinaweza kufikirika sio?
Kipengele hiki bado hakijulikani tarehe rasmi ya kuanza kupatikana kwa watumiaji wote kwani kwa sasa kipo katika hatua za mwanzo kabisa
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani ni huduma gani nyingine ambayo mtandao huo unaweza kuiweka ili kupata mapato zaidi? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.