Tanzania inaongoza kwa sasa katika uagizaji wa magari yaliyotumika nchini Japani kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kusini.
![uagizaji wa magari Japani](https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/uploads/2023/06/port-motor-vehicles.jpg)
Katika data ambazo Kona ya Teknolojia tumefanikiwa kuzipata zinaonesha Tanzania ikiwa nafasi ya nne kwa upokeaji wa magari yaliyotumika yanayouzwa na Japani. Nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Urusi, ya pili na Falme za Kiarabu (UAE) na namba tatu ikichukuliwa na New Zealand.
Data hizi ni za muda wa mwezi wa kwanza hadi wa nne wa mwaka 2023.
![Tanzania inaongoza kwa uagizaji wa magari Japani kwa Afrika Mashariki na Kati](https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/uploads/2023/06/Screenshot-2023-06-08-at-12.34.30-1024x995.png)
Kwa kuangalia data za mauzo ya mwaka jana, ukilinganisha na muendelezo wa mwaka huu inaonekana Tanzania inapokea magari mengi zaidi.
Angalia hapa orodha ya nchi 20 zilizoongoza kwa upokeaji wa magari kwa mwaka 2022, Tanzania ilishika nafasi ya nne, huku Kenya ikiwa nafasi ya tano.
Russia-213,526
UAE- 150,718
New Zealand-84,083
Tanzania-71,651
Kenya- 61,352
Chile- 56,487
Mongolia-46,229
Philippines- 37,411
Malasia- 37,265
South Africa– 36,158
Thailand-35,237
Jamaica- 29,666
Bangladesh- 28,006
Uganda– 26,110
Zambia-19,736
Tanzania inaonekana itaendelea kunufaika kutokana na ukuaji wa mahitaji ya ndani. Orodha hii haihusishi magari yanayopita (IT), bali yanahusisha data za wapi gari linafikishwa (destination) kwa mnunuaji.
Kupata orodha kamili ya mwaka 2022 bofya hapa kuidowload.
Kupata orodha kamili ya Januari hadi April 2023 bofya hapa kuidownload.
Vyanzo: i. Japanese Used Car Auctions Exporter (akebonocar.jp)
Akebono ni kampuni inayohusisha ununuaji wa magari moja kwa moja kwenye masoko ya mauzo ya magari ya ndani ya Japani na hivyo kuwapatia wanunuaji unafuu mkubwa wa bei. Blogu ya Akebono inatoa taarifa mbalimbali muhimu rasmi kuhusu mauzo ya magari ya Japani kwenda duniani kote – BLOGU YA AKEBONO (akebono-akb.com)
ii. Inspection.jp – Shirika la ukaguzi wa magari la nchini Japani
No Comment! Be the first one.