Tuliandika kuhusu ujio wa huduma mbili mpya kutoka mtandao wa 4G LTE wa Smile hivi karibani. Soma taarifa rasmi kutoka kwao kuweza kujua zaidi kuhusu huduma zao mpya; SmileVoice na SmileUnlimited.
Dar es Salaam; Machi 15, 2016. Katika harakati za kuhakikisha wateja wake na watanzania kwa Ujumla wanafikiwa na huduma mtandaoni zenye ubora wa hali ya juu, kampuni ya Smile Tanzania imetengeneza historia nyingine nchini wa uzunduzi wa huduma mbili zinazotumia mtandao wa intaneti wa 4G LTE.
Akizungumzia juu ya uvumbuzi huo katika huduma za intaneti Meneja Mkaazi wa kampuni ya Smile nchini, Bw. Eric Behner, ameeleza kuwa huduma hizo ni SmileVoice inayowawezesha mteja kupiga simu mtandaoni ambayo ni ya kwanza nchini yenye kusikika kwa ubora mkubwa na SmileUnlimited ambayo inatoa fursa kwa mteja kutumia huduma ya intaneti bila kikomo ndani ya siku 30.
SmileVoice ni huduma ya hali ya juu inayopatikana kwenye vifaa vya Android na Apple iPhone kupitia app na kumwezesha mteja kupiga simu mtandaoni ikitumia huduma ya Smile 4G LTE na kumpa mteja uwezekano wa SuperClear voice yaani High definition.
“Smile ni kampuni ya kwanza ya huduma za mawasiliano ya simu duniani kuanzisha na kuendeleza programu ya bure ya huduma ya kupiga simu mtandao wa 4G LTE kutumia app. Huduma hii inawawezesha wateja wetu nchini Tanzania wenye simu za Android na iPhone kufurahia kupiga simu zenye ubora wa hali ya juu kupitia intaneti yetu yenye kasi zaidi.
Tumejizatiti kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha tunaboresha huduma za kupiga simu na mtandao wa intaneti. Kwa kupitia huduma ya Smile Voice, wateja wetu wanaweza kupiga simu nchini na nje ya nchi kama mitandao mingine ya simu.” Alisema Bw. Behner
“Mbali na huduma ya Smile Voice, Smile, kupitia kukusanya rasilimali za kutosha, Smile imefanikiwa kutanua huduma zake mtandao wa 4G LTE mpaka kufikia miji 7 nchini Tanzania na sasa kuwapa fursa wateja kutumia intaneti bila kikomo ndani ya siku 30 yenye kasi zaidi. Hakuna kampuni nyingine nchini inayotoa huduma kama hiyo zaidi ya Smile.” Aliongezea Bw. Behner
Akifafanua zaidi kuhusu huduma ya Smile Unlimited, Bw. Behner amesema kuwa huduma hiyo ipo ndani ya sera ya kampuni ya usawa katika matumizi.
Sera hii itamfaidisha mteja kwani itamuhakikishia kuwa anakuwa ameunganishwa kwa uhakika ndani ya siku zote 30.
Programu ya SmileVoice app inawawezesha wateja ambao hawana simu za VOLTE uhakika wa kupiga simu kupitia mfumo wa LTE wakiwa wameunganishwa na mtandao wa intaneti wa Smile.
“Katika soko la Tanzania, watu wenye vifaa vinavyotumia Android ndivyo vinavyoongoza na ukijumlisha na SmileVoice app, basi tunawahakikishia wateja wetu watakaosajili nasi watajionea na kujivunia upigaji simu zenye ubora wa hali ya juu kupitia simu zao.” Aliongezea Bw. Behner
Ili kuweza kutumia huduma ya Smile Voice, inambidi mteja awe na SIM iliyosajiliwa na akiwa na kifurushi cha Smile. Programu hii inaweza kupakuliwa (downloaded) kwenye simu zinazotumia mfumo wa Android na za iPhone (IOS) na hufanya kazi mara tu baada ya mteja kujisajili nayo mara moja. Wakati simu ikiwa haina intaneti ya mtandao wa Smile mteja anaweza kupiga simu kwenda simu nyingine ambayo imeunganishwa na mtandao wa intaneti wa 3G, Wi – Fi au nje ya nchi.
SmileVoice app – Google Play | iTunes / AppStore