Wengi wetu tumekuwa tunasubiria kwa hamu kuja kwa Windows 10, na baada ya Microsoft kuficha tarehe rasmi kwa muda mrefu mmoja wa washirika (partner) wake wa muda mrefu kibiashara ametoa siri hiyo kwenye akiwa kwenye kikao muhimu. Na kwa kifupi inakuja mwezi wa 7 mwaka huu.
Tayari Microsoft ilishasema toleo hilo linakuja mwaka huu ila ilikuwa bado haijafahamika ni mwezi gani hasa programu endeshaji hii mpya itaweza kupatikana kwa watumiaji wote. Akiwa katika kikao cha mfumo wa simu (conference call) na wadau wa kampuni ya AMD, mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bi Lisa Su alijikuta akitamka ya kwamba toleo hilo la Windows 10 litatolewa mwishoni mwa mwezi wa saba.
[AMD ni kampuni kubwa inayotengeneza vifaa muhimu vya ndani vya kompyuta kama vile CPU na kadi-muonekano (graphic cards)]
‘Mwishoni wa mwezi wa Saba’ – Tegemea kuweza kuipata Windows 10
Toleo la Windows 10 ni tegemeo kubwa kwa kampuni ya Microsoft katika kukuza mauzo yao. Kwani toleo la Windows 7 halikupata mafanikio waliyokuwa wanayataka na wakajikita kutengeneza Windows 8 ambayo ilikuja na mabadiliko mengi sana… nayo haikufanya vizuri kwani ata wale wachache waliohama kutumia Windows XP waliona ni bora kuhamia Windows 7 kuliko 8. Na hadi sasa bado Windows XP ambayo ni ya zamani sana (iliingia sooni takribani miaka 13 iliyopita) inashika namba mbili katika utumiaji baada ya Windows 7 huku Windows 8 ikishika namba 3.
Soma Pia
Je na wewe unasubiria kwa hamu toleo hili la Windows? Unadhani Windows 10 itafanya vizuri zaidi ya Windows 7 na 8?
No Comment! Be the first one.