Habari za kuhusu usajili wa kadi za simu kwa njia ya alama za vidole hivi sasa sio habari mpya tena kwani tumekuwa tukikumbushwa na mitandao ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwenda kukamilisha zoezi hilo mara moja.
Tangu Mei Mosi 2019 zoezi la usajili wa kadi za simu kwa njia ya alama za vidole limeanza na watu kuitikia agizo hilo ambalo lina faida nyingi kwa manufaa ya taifa zima la Tanzania. Miezi minne (4) baadae tangu zoezi kuanza serikali kupitia Wizara husika watafanya tathmini ya zoezi hilo tangu kuanza kwake rasmi mpaka Septemba 30 2019.
Tathmini hiyo itasaidia nini?
Kuwa na takwimu saihi ni kitu muhimu sana katika kuweza kufahamu watu kwa idadi, jinsia, n.k kitu ambacho kinairahisishia nchi kuweza kupanga mipango ya muda mfupi na mirefu kwa maendeleo ya wananchi wake. Kuhusu njia hii ambayo inahimizwa itasaidia kuweza kujua ni nani, kwa kadi ya simu kutoka mtandao gani na anamiliki kadi ngapi za simu kwa usalama wa taifa na wananchi wake. Vilevile, zoezi hilo litasaidia kujua ni nani anayetumia vibaya mitandao ya simu akijaribu kwaumiza Watanzania.

Zoezi hilo litafikia ukomo mnamo Desemba 31 2019 na baada ya muda huo kufika mtu hataweza kutumia kadi yake ya simu lakini tujiulize je, yule mtu mwenye ulemavu asiyekuwa na vidole/mikono atasaidiwaje ili awe kadi yake ya simu isifungwe kwa kushindwa kwenda kusaijili kwa mfumo huu mpya? TUTAFAKARI!.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi