Mmoja wa wasomaji wetu wa teknokona alitaka msaada wa kutatuliwa tatizo lililoikumba Flashi yake kwamba kila akiiweka katika kompyuta yake mafaili yote hayafungui na yanaonekana kama Shortcut.
Ni kweli wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo. Tumeona ni bora kuandaa makala fupi ambayo itawanufaisha wengi zaidi na kuepusha kuombwa utatuzi wa suala hilo mara kwa mara.
Nini sababu ya tatizo la mafaili katika flashi kuonekana kama Shortcut?
kinachosababisha ni Virus ambaye anachofanya kubadili mafile katika Flash. Ni kwamba Virus anakuwa ameingia katika Flashi na kusababisha file zako kuwa katika namna ya Shortcut.
Na hii hutokea pale Flashi inapowekwa katika kompyuta iliyoathiriwa na Virus. Nini cha kufanya hali hiyo inapotokea katika Flashi yako. Unachotakiwa ni kuiingiza katika Kompyuta yako kama kawaida na kisha futa hatua ya kwanza mpaka ya tano kama tulivyoelekeza hapo chini.
Fanya hatua zifuatazo:-
1. Angalia Flashi imesoma herufi gani kama ni D, E, F, H, n.k
2. Baada ya kujua herufi iliyosoma fungua RUN (Windows + R) na andika CMD kisha bonyeza OK
3. Ikishafungua andika herufi inayosoma Flashi yako na uweke alama ya Colon : Mfano D:
4. Baada ya hapo andika attrib *. -h -s /s /d kisha bonyeza Enter
5. Subiri kwa sekunde kadhaa ikimaliza nenda kafungue Flashi yako utakuta file zipo kama kawaida.
Ukifuata hatua hizo kwa ufasaha utakuwa umemaliza tatizo la mafaili yako kuwa katika Shortcut. Ili tatizo hilo lisijirudie hakikisha Flashi yako unaitumia katika kompyuta zilizo salama na mashambulizi ya Virus.