Mwanamuziki wa kimataifa Taylor Swift ana mipango ya kuletagemu la kwenye simu janja mwishoni mwa mwaka huu. Msanii huyo wa mtindo wa Pop atashirikiana na kampuni ya Glu Mobile katika kuandaa mchezo (Gemu) huo.
Gemu hiyo itatoka rasmi mwishoni mwa mwaka 2016. Inaonekana wazi kwamba tuanze kufikiria mafanikio makubwa zaidi ya Taylor Swift katika ulimwengu wa kidigitali. Kumbuka hata katika mtandao msanii huyu anafanya vizuri sana.
Taylor Swift alisema ataungana na Glu Mobile katika kutengeneza Gemu ambalo litakuwa ni bure kabisa kucheza. Ambalo pia litakuwa ni moto wakuotea mbali kwani mtu yeyote angetegemea gemu hilo kuwa nzuri hata ingekuwa kwa msanii mwingine mkubwa yeyote.
Taylor Swift ana mashabiki (fans )milioni 74 katika mtandao wa kijamii wa Facebook, Milioni 64.8 Katika Instagram, milioni 70.4 katika Twitter na watu milioni 8 katika katika akaunti yake ya Vevo katika mtandao wa Youtube.
Taylor Swift ana takribani nyimbo milioni 130 ambazo zimeshushwa duniani katika mitandao maarufu na mauzo ya albamu milioni 40. Na kwa sasa albamu yake ya 1989 inagombea tuzo za albamu ya mwaka katika tuzo za Grammy. Pia anagombea vipengele 7 katika tuzo hizo mwaka huu (2016)
Kama kawaida Glu Mobel imefanikiwa sana kwa kutengeneza gemu za watu maarufu. Kwa mfano kampuni la Glu limtengenezea Gemu la Kim Kardashian ambalo lilikuja kuwa lenye faida sana. Gemu hilo liliingiza dola za kimarekani milioni 43 kwa miezi yake mitatu tuu ya mwanzo.
Gemu hili la Taylor Swift kuna hati hati likawa lipo kama video ya ‘Blad Blood’ ya msanii huyo. Kampuni la Glu limeahidi kuwa litaongeza manjonjo na mbwembwe katika ushirikano na msanii huyo wa kutengeneza gemu hili.
Uzuri wa jambo hili ni kwamba, Mwana dada Taylor Swift hatopata tabu kwani kulingana na network aliyonayo anaweza kulitangaza Gemu hili na likapata watu wengi wa kulicheza (ndani ya muda mchache).
No Comment! Be the first one.