Mamlaka ya mawasiliano Tanzania almaarufu kama TCRA imeweka wazi na kusema kuwa tangia waseme kama wamebakiza muda mchache ili kuanza kufungia simu ambazo ni feki kuna mambo yamebadilika. Hii ikiwemo na asilimia ya kumiliki simu feki kushuka.
Kuna kipindi mamlaka hiyo ilisema kuwa kwa Tanzania asilimia 40 ya watu wanatumia simu feki. Namba imeshuka kwa sababu watu wanaogopa na hivyo inawalazimu wawe na vifaa ambavyo vinatambulika (Origino)
Kampuni limesema kuwa namba hiyo imepungua kwani siku hizi watu wako makini sana. Hii zoezi hilo watu wengi hulifanya mwanzo kabisa kabla ya kufanya kitu chochote.
“Watu wanakagua vifaa vyao kabla ya kuvinunua ili kuhakikisha kwamba ni origino au la” – Alisema mkurugenzi wa TCRA, Bw. Ally Simba
Pia aliongezea kuwa jambo hili linasambazwa sana kadri iwezekanavyo kwa watu ili wajue kabisa kuwa mpka tarehe 16 mwezi wa 6 ndio inategemewa kuwa mwisho wa kutumia simu zote ambazo sio origino
Kuhusu swala la simu kuwa origino au la watu wanachanganya sana. Kuna wale ambao wakiona simu za kichina tuu wanaogopa na kuanza kusema simu hizo ni feki
Hapa cha msingi ni kuchukua simu yako na kutuma ule ujembe kwenye TCRA ili wakujulishe kama simu yako ni feki au iko vizuri
MUHIMU: Kujua Kama Simu Yako Ni Feki Au La – Bofya Hapa.
TCRA vile vile ina mpango mkubwa sana wa kusadia watu kupitia na zoezi hili. Kwa mfano kama simu feki zote zikipigwa chini itakuwa ni rahisi hata kusaidiwa unapopata tatizo. Tatizo kama lile la kuibiwa kifaa chako. Licha ya kuwa siku hizi simu janja zetu zina mambo mengi kiasi cha kwamba hata zikiibiwa bado tunaweza kuwa na njia kadhaa za kuzifikia. Naamini TCRA wanaweza wakarahisisha zaidi zoezi hilo.
Chanzo: Daily News