Kuna wasomaji waliotaka kujua sifa za Tecno M3 na P3, na wengine walitaka kufahamu tofauti zake, hivyo leo tunakuleta uchambuzi mdogo juu ya simu hizo. Tunategemea inaweza kuwasaidia wengine wengi waliokuwa wanafikiria kununua simu hizi.
Kwa kuanzia simu zote mbili ni simu janja za kiwango cha chini na hivyo ni za bei rahisi. Je zinafaa kwa matumizi ya kila siku hii ikiwa ni pamoja na intaneti? Jiunge nasi kujionea mwenyewe.

Kiufanisi;
Kwanza kwenye eneo la programu endeshaji simu zote zinatumia Android, Tecno M3 inakuja na Android 4.2 (Jelly Bean) wakati Tecno P3 ina toleo la zamani la Android nalo ni Android 2.3 Gingerbread. Hivyo hapa kulingana na pesa yako chaguo linatakiwa kuwa Tecno M3.
Je ipi in a nguvu zaidi? Kwenye suala la prosesa, Tecno M3 ndiyo ipo juu zaidi ukilinganisha na Tecno P3 kwani M3 ina prosesa ya 1GHz Dual-core wakati P3 inaprosesa ya 1Ghz.
Kiwango cha RAM je? Simu zote mbili zinakiwango cha kawaida cha RAM ya MB 512. Kumbuka kiwango chochote cha chini ya GB 1 kwenye la RAM ni kiwango kidogo na cha kawaida ila kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya apps za kawaida ni kinachotosha.

Kioo na Muonekano (Display)
Simu zote mbili zina kioo cha ukubwa wa inchi 3.5, na ‘resolution’ ya pixels 320×480.
Kamera
M3 ndiyo yenye kamera bora zaidi, kamera yake ya nyuma ni MegaPixel 5 wakati ya mbele kwa ajili ya selfi ina MegaPixel 0.3. Tecno P3 kamera yake ya nyuma ni MegaPixel 3 na ya nyuma ni megapixel 0.3.
Diski Uhifadhi (Storage)
Tecno M3 ina GB 4 kwa diski ya ndani, wakati Tecno P3 inakiwango kidogo cha GB 512 tuu. Simu zote zinakubali SD Memori Kadi, na zinakubali memori kadi za hadi GB 32.
Mawasiliano
Simu zote zinakuja na uwezo wa kutumia laini mbili. Zina teknolojia ya Bluetooth, WiFi na pia unaweza kutumia waya wa USB. Simu zote zinakubali teknolojia za 2G na 3G. Ila kwenye M3 utaweza kupata intaneti ya kasi zaidi kwani inauwezo wa kupokea signo za intaneti hadi za 3.75G.
Betri
Kiwango cha betri ni kimoja kwenye simu zote mbili, nacho ni 1,400mAH, na kiwango hichi ni cha kawaida kwa matumizi madogo.
Sifa zinginezo
- Zote zinamakava ya plastiki.
- Unaweza ukacheza vigemu mbalimbali vizuri kwenye M3 kuliko kwenye P3.
- Kote utaweza kutumia ‘ear phones’ na kusikiliza muziki kama kawa.
- FM Redio kwenye simu zote mbili inapatikana
BEI?
Bei zake hazitofautiana sana inategemea zaidi na mahali unaponunua. Bei zinazocheza kati ya Tsh 110,000/= hadi Tsh 150,000/= kwa uchunguzi wetu, ila unaweza kutuambia kupitia kwenye ‘comment’ chini kama unafahamu mahali unapofahamu bei zake kwa sasa.
Je ununue ipi?
Hapa itategemea bajeti yako kipesa, ila tambua simu hizi si kwa watumiaji wakubwa sana wa simu janja. Ni matoleo ya kawaida sana, ila kwa kuzilinganisha kama unaitaji kununua moja wapo basi sisi tutakushauri ununue Tecno M3.
Habari, sorry naomba unisaidie kunipatia tofauti kati ya tecno M3 na tecno H3