Tecno Pova 6 Pro 5G ni simu mpya iliyotangazwa na Tecno. Hii ni simu yenye muonekano wa kitofauti kwa nyuma, hii ikiwa na pamoja na utumiaji wa teknolojia ya taa za LED kama vile zilivyotumika kwenye simu za Nothing Phone.

Hebu tuiangalie kwa undani:
Muundo:
- Ndani ya Boksi: Pova 6 Pro inakuja na ‘earphones’, chaja, kebo ya USB, na kasha la kinga (Cover).
- Taa za LED: Nyuma ya simu kuna taa za LED, ikiwa ni pamoja na taa zilizopangwa kwa umbo la duara karibu na lensi moja ya kamera na taa ndefu yenye umbo la Y. Taa hizi zinaweza kubadilishwa kwa mitindo mbalimbali na hata kutoa ishara kwa simu, arifa, muziki, au kuwaka kwa muda mrefu (ingawa inaweza kutumia betri kidogo).
- Skrini ya AMOLED: Mbele kuna skrini kubwa ya AMOLED ya inchi 6.78 na kiwango laini cha kuboresha cha 120 Hz.
- Muendakano wa Kuvutia kwa nyuma: Nyuma ya simu kuna ubunifu wa muonekano wa kuvutia wenye uwezo wa kuakisi (reflect) mwanga.
Uwezo:
- Prosesa: Inakuja na chipset ya MediaTek Dimensity 6080 na RAM ya GB 12. Tarajia utendaji wa haraka kwa matumizi ya aina mbalimbali kama vile games/michezo nk.
- Programu Endeshaji: Android 14 ikiwa na muonekano wa Tecno HiOS.
- Kamera kuu ya Megapixel 108. Ingawa kuna lensi tatu nyuma, simu inatumia kwa kiasi kikubwa kamera yake kuu ya Megapixel 108. Pia ina uwezo wa kuzoom wa 3x.
- Kamera ya Selfie ya Megapixel 32.
Betri:
- Kwenye betri Tecno Pova 6 Pro 5G inahakikisha unaweza kuitumia muda mrefu bila uhitaji wa kuchaji kutokana na uwepo wa betri la kiwango cha juu cha mAh 6,000.
- Chaja ya 70W: Inatumia USB Type C kuchaji, ikiwa na kiwango cha uwezo wa kuchaji kwa haraka wa 70W.
Bei: Toleo la RAM GB 8 / Diski Uhifadhi wa GB 256 inategemewa kwenye bei ya dola 229 – takribani Tsh 600,000/=, wakati toleo la RAM GB 12/ Diski Uhifadhi wa GB 256 kwa bei ya dola 269 – takribani Tsh 700,000/=. *Bei inaweza kupanda kutokana na sababu za kikodi na biashara.
Simu hii inategemewa kuanza kupatikana mwezi Machi 2024, ikianza kuuzwa katika nchi za Ufilipino, Saudi Arabia, na India kabla ya kuanza kupatikana katika masoko mengine duniani kote.
Vyanzo: GSM na vyanzo mbalimbali
No Comment! Be the first one.