Tunaweza tafuta njia mbadala ya kuonyesha Msisimko wetu wakati wa kutuma meseji na kuchati katika vifaa vyetu vya elektroniki. Kutuma meseji kwa kutumia Emoji (Zile alama za rangirangi kama sura ya furaha, ukauzu, kununa, dole gumba n.k) inaweza fanya meseji ikaonekana nzuri zaidi. Mfano ukituma meseji ya kuchekesha alafu mtu akakujibu ujumbe akaweka na zile emoji za sura ya kucheka ukiachana na ‘hahahahahaha’ inakua inavutia zaidi.
“Watu wote duniani wanahitaji Emoji ambazo zinafanaa zaidi na watu hasa hasa katika swala la rangi za ngozi” Unicode waliandika katika ripoti yao
Ripoti hiyo ni rasimu ya baadae kuhusina na mipango ya kundi hilo kuhusina na Emoji, kwa hiyo inaweza ikabadilika kabla ya mwezi julai mwaka ujao. Unicode imekua ikipoke shinikizo kwa watu mbali mbali na hata kampuni ya Apple kwamba inabidi itengeneze Emoji ambazo kidogo zinafanana na watu wanaozitumia.
Emoji zenye sura mbali mbali zinakuja kabla ya mwezi julai 2015 na hii habari ni kutoka kwa Unicode (kundi la watu wanaosimamia Emoji). Aina 5 tofauti za ngozi zimepangwa kuwepo katika ‘Update’ ya software ya Unicode katika Emoji zinayokuja.
Emoji ambazo zimezoeleka sasa ni zile za watu wenye ngozi nyeupe. vipi kuhusu ngozi nyeusi na zingine? Emoji mpya zitakua na mabadiliko hata kwa rangi za nywele na hii inavutia zaidi!.
Hii ni taarifa nzuri kwa wale wanao lalamika kuhusiana na Emoji kukosa rangi za ngozi mbali mbali. Ukiangali Emoji ni njia mpya ya siku hizi ya watu kuwasiliana, badala ya kuandika maneno unaweza tuma emoji. Wewe umeipokea vipi taarifa hii?? Tuammbie katika Facebook Page Yetu na pia tembelea Instagram Page yetu
Siku Njema!!!
No Comment! Be the first one.