Taasisi isiyo ya kiserikali (NGO) inayojulikana kama Internet Society imeialika timu ya TeknoKona katika tukio lake kubwa na la aina yake. Tukio ambalo ni la saba duniani linalokwenda kwa jina la ‘The 7th African Peering and Interconnection Forum (AFPIF)’
Moja kati ya malengo ya tukio hili ni kukutanisha watu na kutoa fursa mbalimbali huku wakiunganisha watu bila kushahau makampuni na wateja wao, ambayo yamepewa mualiko katika tukio hilo.
Tukio hili linachukua nafasi tarehe 30 mwezi agosti mpaka tarehe moja mwezi septemba.. Maelezo zaidi yapo hapa
Moja kati ya mambo ambayo TeknoKona iliuzwa ni kwamba kwanini matumizi ya intaneti kwa nchi za Africa yanashuka? – majibu yalikuwa kama ifuatavyo
Ukosefu wa elimu
Tuwe wakweli ni wazi kwamba waafrika wengi (Watanzania) hawana elimu ya kutosha kuhusiana na intaneti. Usijifikirie wewe tuu, fikiria Yule mtu pengine ambae yupo kijijini. Kumbuka elimu hiyo ndio baadae inaweza ikaleta maarifa. Kwa kutumia Intaneti hiyo ndipo mtu anapoweza kufanya mambo mengi kama vile kutumia intaneti katika kufanya biashara zake na kuweza kujitangaza zaidi na mengine mengi ambayo yanaweza yakatoka na intaneti.
Miundombinu Mibovu
Fikiria ni mara ngapi wamesema intaneti unayotumia ni 3G au 4G lakini kwa tathimini yako ya kawaida tuu unaona kwamba hilo ni uongo?. Ukiachana na hilo ni mara ngapi ulipata zile meseji za ‘Samahani kwa usumbufu uliojitokeza kuna tatizo la kiufundi”? – nadhani majibu unayo. Wakati dunia inakimbilia katika kuhakikisha inawezesha Teknolojia ya 5G sisi ndio kwanza tumeganda katika 3G na 4G kwa mbali
Gharama Kubwa
Unaweza ukanitaji Gharama ya bando unalonunua ili kulitumia kwa mwezi? Kwa nchi za Afrika kumbuka nyingi ni maskini sana hivyo chakula huanza kwanza na mambo mengine ndipo yafuate. Kumbuka wengi kwa Tanzania wanaishi chini ya dola moja, hivyo mtu hawezi kufikiria kununa bando wakati hajala.
Mtazamo Hasi
Vile vile watu wanatofautiana mtazamo, kuna wengine wanachukulia kama kutumia intaneti ni jambo la ‘kishua’ – maskini wengi wanaweza wakaniunga mkono – lakini si kweli kwani watu wanakua tuu na mtazamo huo ambao sio chanya.
Hapa vitu vya kufanya ili kuongeza matumizi ya intaneti katika nchi za Afrika nafikiri moja wapo itakuwa ni kutoa elimu kubwa juu ya intaneti ni kwa kiasi gani inaweza kuwasaidia watu katika shughuli zao za kila siku. Vile vile gharama inabidi zishushwe.
Nilikua nikiongea na mtu akasema gharama ni kubwa sana, hebu fikiria unaweza ukanuna kifaa chako (simu au kompyuta) lakini ili hicho kifaa ukifaidi vilivyo huna budi kuweka bando mara kwa mara ila kukitumia vizuri. Na kumbuka kama huna intaneti katika kifaa chako huwezi kukifurahia kama ukiwa nayo. Vipi gharama kwa ujumla ukishushwa? Mambo yatakuwa poa!
Pia TeknoKona ilipata nafasi ya kushirikiana katika mazungumzo na Bi. Lia Kiessling na Bw. Bastiaan Quast ambao wanatokea katika taasisi isiyo ya kiserikali (NGO) inayojuliakana kama Internet Society. Mazungumzo hayo yalikuwa yanahusisha juu ya kwanini mitandao mingi haiandiki habari zake kwa lugha mama.
Kwa mfano kwa Tanzania unaweza ukakuta kuna tovuti (site) nyingi ambazo zinaandikwa kwa lugha ya kiingereza wakati wasoma wengi wanaowategemea ni watanzania. Kumbuka kuna baadhi ya watanzania wanashindwa soma maandiko hayo kwa sababu ya lugha (lugha gongana hahah). TeknoKona imekuwa ni mfano wa kuigwa kwani tunatumia lugha mama ili kila mtu aelewe kinachoandikwa.
Mengi yameelezewa hapa kuhusiana na tovuti kutoa maandiko katika lugha mama ili wengi waweze kuelewa. Kumbuka kuwa na intaneti pekee hakumfanyi mtanzania wa kawaida kuingia katika mtandao Fulani. Lakini kama mtandao huo utakuwa unaweka vitu vyake katika lugha ya Kiswahili itakuwa ni rahisi kwa yeye kuingia katika mtandao huom kusoma na kuelewa vitu na pia kurudi tena baadae katika mtandao huo huo. Unaweza ukasoma zaidi hapa na kusikiliza maelezo ya Bw. Divine
Kama ukitaka kushudia ‘Live’ Bw. Bastiaan Quast akiongea (tarehe 1 septemba) huna budi kuwa katika mtandao huu kuanzia saa tano kamili (asubuhi) na utaweza ku’Live Stream’ maongezi yake (Video) yote hapa
Tuambie hivi wewe unadhani ni sababu zipi ambazo zinapelekwa amtumizi ya Intaneti kushuka kwa nchi – usijiangalie wewe tuu angalia swala hili kwa upana – za Afrika. Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment.