Inaweza ikawa ni miujiza kwako kama ni mgeni wa teknolojia, lakini kama ni mzoefu wa mambo haya utasema —nlijua tuu!— Kampuni ya SanDisk licha ya kuwa kampuni ambayo inasifika sana kwa kutengeneza vifaa vyenye uwezo
wa kuhifadhi kumbukumbu (memory) kama vile memori kadi na flash. Bado ni kampuni ambalo linatoa vitu vyenye hadhi ya teknolojia ya kisasa. USB Diski hii vile vile inatumia chaji ya kujitegemea yaani bila hata ya umeme inafanya kazi (Kama ikichajiwa) kwa muda wa masaa manne na nusu tangia ichajiwe.
MIUJIZA NDANI YA USB DISKI HII
- Pata mafaili yako bila kutumia waya au hata internet
- Bila kutumia waya waweza ‘save’ na kutembelea mafaili yako
- Unaweza ‘share’ mafaili yako hata kwa marafiki zako
- Unaweza uka ‘stream’ video mpaka kwa vifaa vitatu kwa wakati mmoja (lakini USB Diski hiyo iwe karibu tuu Mfano nyuma ya siti)
- Uwezo wa ku ‘back up’ picha zako katika ‘camera roll’ automatiki
- USB Diski hii inauwezo wa ku ‘save’ kuhamisha na pia kuonesha mafaili katika kifaa chochote chenye WiFi hii inajumuisha iOS na Android, Amazon Fire tablets, Macs, na kompyuta. Pia unaweza chomeka katika kompyuta yako ili kutuma na kuhamisha mafaili kiurahisi zaidi.
App ambayo itakusaidi kutumia USB Diski hii unaweza kuiipata katika App Store, Google Play store, na Amazon Appstore na ni bure kabisa
Pia kifaa kinapatikana katika uwezo wa 16GB, 32GB, 64GB, and 128GB kutoka Amazon, BestBuy.com, na SanDisk.com
Angalia Video Fupi Inayoelezea USB DIski hii
[iframe id=”https://www.youtube.com/embed/TaCjquOZPPI” align=”center”]
No Comment! Be the first one.