Kampuni ya kikorea ya LG imekuja na keyboard maalumu kwaajiri ya simu janja na tableti, keyboard hiyo ambayo inakunjika na kuwa kama kifimbo hubebeka kirahisi zaidi. Keyboard hii ni ya mfumo wa QWERTY na ina kila kitufe ambacho kipo katika keyboard za kawaida.
LG wameipa jina la “Rolly Keyboard” keyboard hiyo kutokana na uwezo wake wa kujikunja ambao ndiyo sifa ya kuiuzia bidha hiyo. Ikiwa ni ndogo kuliko keyboard za kawaida, kila kitufe kinachukua 17mm (kama ulikua hujui keyboard ya kawaida kitufe kinachuka 18mm).
Rolly keyboard inatumia seli kavu (baterry) za ukubwa wa AAA na hii seli inakadiriwa itadumu kwa miezi mitatu kwa matumizi ya kawaida. Rolly inaungwa na simu janja na tableti yako kwa kutumia bluetooth. Sifa hizi zinaifanya keyboard hii kuwa suluhisho kwa waandishi wa kizazi hiki cha simu janja ambao sasa wataweza kuandika habari ndefu hata wakiwa na simu zao.
Rolly keyboard itazinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa tisa na moja kwamoja itaingia katika maduka ya Marekani, kwa nchi nyingine keyboard hii itaanza kuuzwa baadaye kidogo. LG wanatoa bidhaa mbili katika robo ya mwisho ya mwaka rolly keyboard na toleo jipya la tableti yake ya G Pad na wanategemea bidhaa hizi mbili zitasaidia kuleta faida baada ya kupata hasara katika kipindi kama hiki mwaka jana.
Je una mtazamo gani juu ya habari hii? Tungependa kusikia kutoka kwako.
No Comment! Be the first one.