Ukuaji wa teknolojia katika baadhi ya nyanja kama za teknolojia ya wasiliano umekuwa kwa kasi sana ukiinganishwa na sekta zingine za vitu tunavyovitumia kila siku kama vile viti, ila mambo yanabadilika kwa sasa. Miaka ya karibuni kumejitokeza baadhi ya watu wanaojituma katika kufanya mabadiliko haya kupitia ubunifu na utumiaji wa teknolojia kuleta maboresho katika baadhi ya vitu tulivyovizoea kama vile viti vya kukalia na masuala yote yahusuyo ukaaji.
Kuna makampuni mawili ambayo yanaongelewa sana kwa sasa katika ubunifu wao wa kiteknolojia katika kuraisisha ukaaji ata pale ambapo kukaa ingekuwa ni kwa shida au ni vigumu.

NOONEE
Kampuni namba moja inafahamika kama Noonee kutoka jiji la Zurich huko Uswizi. Hawa wanatengeneza viti ambavyo vimepewa jina la utani la ‘viti visivyoonekana’ – (invisible chairs), wenyewe Noonee kimombo wanaviita ‘Chairless Chair’.
Je, vikoje?
Havipo kama viti ulivyovizoea, hapa unavaa vyuma vilivyojengewa na programu yake kwa ajili ya kuweka ugumu wa wewe kuweza kukaa pale utakapoitaji. Ukiwa umevaa vyuma hivyo pamoja na kufunga mikanda katika maeneo ya mapaja na kiuno, utaweza kubonfya sehemu pale unapoona umepiga pozi unalotaka kukalia na basi tayari vyuma hivyo vitajikaza na kuweza kukuruhusu kukaa bila shida wala kuanguka.

Mfumo huo unakuja na viatu vyake ambavyo navyo ni sehemu ya mtambo mzima wa viti hivyo. Pale unapozima mfumo huo, bila ata kuvua utaweza kutembea na kukimbia bila shida yeyote. Kupitia sayansi ya jinsi ya kucheza na mienendo ya uzito kifaa hicho kinaweza kuhamisha uzito wa mtu pale unapokaa kuupeleka kwenye eneo la viatu hivyo kukuwezesha kuweza kukaa ata katika mazingira ambayo ingekuwa si rahisi wewe kuweza kukaa.
Matumizi?
Viti hivi unaweza kutumia katika mazingira yeyote ile yenye shida au ugumu wa viti au pahali pa kukaa, ila kwa kiasi kikubwa teknolojia hii imetengenezwa kwa ajili ya wafanyakazi wa viwandani. Viwandani viti vinajaza nafasi na pia pale panapokuwa na viti muda mwingi unapotezwa katika kuvisogeza sogeza kila mara, pia kwa viwanda visivyotumika viti kwa ajili ya nafasi basi wafanyakazi huwa wanawahi kuchoka na hivyo uzalishaji unakuwa mdogo. Teknolojia hii imekuja kutatua hilo! Ila ata kwenye daladala unaweza tumia hii kitu ati… 🙂

Bei? – Bado hawajaweka bei wazi.
VITRA
Vitra kutoka Marekani ni kampuni nyingine katika suala la teknolojia ya ukaaji. Wakati NOONEE wamejikita katika teknolojia iliyoitaji nguvu za kipesa na kiteknolojia zaidi teknolojia ilinayotumiwa na Vitra ni rahisi na inayoweza kukopiwa na makampuni mengine kirahisi zaidi.
Kipoje?
Huu unakuwa ni mkanda mnene mnene ambao utajizungushia pale utakapokaa chini, unaweza kuuweka sawa (adjust) hadi pale unapoona umekaa vizuri zaidi. Mkanda huu utaweza kukusaidia kuweza kukaa chini kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida bila kupata maumivu kama ya mgongo na mapaja.
Mbunifu wa mikanda hii Bwana Alejandro Aravena wa Vitra amesema alipata wazo hili la ‘kiti kisicho na miguu’ alipokuwa nchini Paragwai (Paraguay) ambapo alimuona mtu wa asili ya huko, kijijini, akitumia kitu flani kinachofanana na ubunifu huu. Hadi sasa kwa kila mauzo ya mikanda hii Vitra wanatoa kiasi flani cha pesa kwa ajili ya kusaidia shirika la kibinadamu la kuleta maendeleo katika nchi hiyo.
Matumizi
Kwa kiasi kikubwa teknlolojia huu kutoka kwa Vitra ni kwa matumizi ya kawaida ya kila siku ya watu wa aina mbalimbali kama mimi na wewe. Unakumbuka mara ngapi umeshaenda kukaa sehemu kama ufukweni au bustanini ikakubidi kusimama kwa sababu ya kumaliza aina ya mikao kutokana na maumivu ya mapaja? Basi hii itatua. Pia yale mambo yetu ya mkekani kibongo bongo basi kwa kutumia hii kitu utaweza ata kukaa siku nzima bila maumivu ya mgongo wala mishipa ya mapaja.

Bei? – Ni kwa Dola 30 za Marekani (Takribani Tsh 52,000/=)
No Comment! Be the first one.