Kufuatia ajali kadhaa kwa magari ya Tesla yakiwa katika mfumo wa kujiendesha yenyewe kampuni hiyo hatimaye inafanyia madiliko mfumo wake wa kujiendesha wenyewe.
Magari ya kampuni hii yanao uwezo wa kujiendesha yenyewe ambao gari hujiendesha lenyewe inapowashwa na huwa na uwezo wa kukata kona kupunguza mwendo ama kusimama kulingana na hali halisi ya barabarani. Hata hivyo kumekuwa na ajali kadhaa ambazo zinatokea nyakati ambapo mfumo huu wa kujiendesha wenyewe ukiwa umewashwa.
Tesla wamesema baadhi ya ajali ambazo zimetokea haikuwa kosa la mfumo wa kujiendesha wanadai nyingi zinatokea kwasababu watumiaji ama wanadharau masharti ya utumiaji wa huduma hiyo au wanaitumia isivyo, hata hivyo katika ajali moja iliyotokea mwezi Mei ambapo dereva wa gari la model S alifariki baada ya gari hilo ambalo lilikuwa katika mfumo wa kujiendesha kugonga trekta. Tesla walikubali kwamba mfumo wa gari kujiendesha lenyewe ndio ulio kuwa na makosa katika ajari hiyo ya Mei 7, na hii ndio imepelekea kampuni hiyo kufanya mabadiliko katika mfumo huo.
Tesla wanasemaje juu ya tatizo katika mfumo wao wa gari kujiendesha?!
Kwa mujibu wa wataalamu ripoti ya kampuni hiyo kunauwezekano wa kwamba Radar ya gari hilo ilishindwa kulitambua tela la trektor hilo hivyo kushindwa kusimamisha gari na hatimaye ajari ikatokea.
Kampuni hiyo inafanyia mabadiliko wa mfumo huu ili kuweza kuboresha namna ambayo radar kamera na sensor zinawezakugundua vitu barabarani na hatimaye kuzuia ajali.
Hii inamaana gani katika sekta ya magari ya kujiendesha?!
Kampuni hii ni moja kati ya makampuni ambayo yapo mstari wa mbele katika kuleta teknolojia ya magari yanayojiendesha hivyo mabadiliko yoyote yatakayofanywa na kampuni hii yatakuwa na ushawishi kwa makampuni mengine katika sekta hii.