Threads ni moja kati ya mtandao wa kijamii mpya ambao ujio wake uliwaacha watu katika mshangano, na ni wazi siku yake ya kwanza ulipata watumiaji wengi sana.
Mtandao huo wa Threads unamilikiwa na Meta ambao wanamiliki mitandao mingine ya kijamii kama vile WhatsApp, Instagram na Facebook.
Kilichotokea ni kwamba mfanyakazi mmoja wa Meta kwa bahati mbaya amevujisha Screenshot ya kipengele hiki ambacho kinategemewa kutoka katika mtandao huo.
Kipengele hichi ni sehemu kubwa ya kuonyesha ni mambo gani yamechukua vichwa vya habari na yanaongelewa kwa ukubwa kuliko vitu vingine.
Nadhani ushawahi sikia kwamba mtu Fulani au kitu Fulani kimetrend, moja kwa moja mpaka kufikia huko inamaanisha unazungumziwa sana.
Mapokezi ya watu kwa taarifa hii ni kwamba mtandao wa Threads unaiga kipengele hicho kutoka katika mtandao wa X (Zamani Twitter).
Wengine wameenda mbali Zaidi na kupongeza kwamba ni sawa kwa mtandao huo kufanya hivyo maana unaleta ushindani wa hali ya juu na kingine ni kwamba kipengele hicho hakipo katika mtandao wa X tuu.
Kwangu mimi hili ni jambo jema kote kote, ni nzuri katika ushindani na ni nzuri kwa mtandao wa Threads kuwa na kipengele kipya..hii inaonyesha ni jinsi gani mtandao unakua.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika sehemu ya comment, je hii umeipokeaje? Unadhani dhamiri ya Threads ni kuchukua kipengele cha mwenzake?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.