Mtandao wa kijamii wa Threads watoa toleo la kutumika kwenye vivinjari, baada ya kupatikana kupitia toleo la app. Swali lililopo kwa wengi je, uamuzi huu utaweza kuuokoa mtandao huo wa kijamii dhidi ya kuporomoka kwa watumiaji wake?
App ya Threads iliyoletwa kushindana na mtandao wa kijamii wa Twitter, ambao kwa sasa unafahamika kwa jina la X, ilivunja rekodi ya kihistoria ya kupata watumiaji wapya.
- Meta, wamiliki wa Facebook na Instagram, walizindua app ya Threads kwa watumiaji wa Android na iOS Julai 5
- Akaunti mpya milioni 100 zilifunguliwa ndani ya siku 5, na idadi ilifikia milioni 150 ndani ya siku 7.
Mafanikio yalikuwa ya muda mfupi kwani kuanzia mwezi mmoja baada idadi ya utumiaji wa app hiyo ukashuka sana.
- Mfano kwa watumiaji wa Android, wastani wa watumiaji kwa siku umeporomoka kutoka watumiaji milioni 49.3 kila siku hadi kufikia watumiaji chini ya milioni 10 kwa siku.
- Pia wastani wa muda ambao watumiaji wanautumia kwenye mtandao huo wa kijamii umeporomoka sana, kutoka wastani wa zaidi ya dakika 20 hadi chini ya dakika 10.
Ukilinganisha mtandao wa X (Twitter), unatembelea na wastani wa watu;
- Threads – Wastani wa watumiaji milioni 8 kwa siku, kila mtumiaji anatumia wastani wa dakika 2.9 kwa siku.
- Twitter – Wastani wa watumiaji milioni 100 kwa siku, kila mtumiaji anatumia wastani wa dakika 25 kwa siku.
Bado ni mapema sana kuona kama mtandao wa kijamii wa Threads unaweza kujiokoa kutoka kwenye anguko la idadi ya watumiaji wa mara kwa mara wa mtandao huo.
Muda utatuonesha, kwa sasa unaweza tembelea tovuti ya Threads kupitia anuani yake ya www.threads.net
No Comment! Be the first one.