Threads ndio mtandao wa kijamii ambao umekuja na kuvunja rekodi kwa kupata watumiaji wengi ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Ukaichana na namba hiyo ya watumiaji wengi wanaushinikiza mtandao huo kwamba umenakili muonekana na unatumika kama inavyotumika Twitter.
Kwa kupitia hilo Twitter imetishia kwamba itaifungulia kesi kampuni hiyo kwa sababu ni kweli kwa haraka haraka kuna mfanano.
Thread inamilikiwa na kampuni ya Meta, ni kampuni mpya chini ya kampuni hilo kubwa linalomiliki mitandao mingine kama vile Facebook, Instagram na WhatsApp.
Kumbuka watu ambao wako katika mtandao wa Instagram wana uwezo wa kuingia katika Threads kwa kutumia akaunti zao za Instagram.
Kingine kikubwa zaidi ni kwamba akaunti hizo zinaweza mpaka kubeba wafuasi (Followers) wa Instagram na kuwafanya wawe wa Threads.
Kwa mfano akaunti ya TeknoKona kupitia Instagram kama itajiunga na Threads basi itaondoka na Followers wake wote —-lakini ni mpaka na wenyewe wawe wamejiunga na mtandao huo wa Threads maana sio wote huwa wanajiunga na mitandao mipya
Kwa haraka haraka ukifikiria mtandao huu umepata watu wengi waliojiunga nao kwa sababu ya urahisi wake wa kujiunga alaf kingine ni kwamba hauanzi na moja kabisa.
Kumbuka mitandao mingi ili kujiunga ni mpaka ujaze fomu ndefu, mara mambo ya kuweka picha na kuuandaa taarifa katika ukurasa wako.
Wakati katika Threads unaweza tumia ukurasa wako wa Instagram na kuhama na Taarifa zako zote na kuzitumia katika ukurasa wa Threads (ni kama umezinakili tuu).
Wengi kwa sasa wanashindanisha mtandao wa Threads na Twitter huku watumiaji wengi wa Twitter wakihamia katika mtandao huu mpya moja kwa moja.
Kingine ni kwamba wataalamu wengi wa mambo wanasema katika dunia ambayo tumefikia ni ya aina yake kama kampuni linaweza anzisha mtandao mwingine na kuhamishaa na taarifa za mtandao wa zamani na kuzipeleka katika mtandao mpya ni kitu cha kushanganza sana miaka ya nyuma akili hii haikuwepo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa maoni je unadhani mtandado huu utazidi kukuwa na kupitia watumiaji wa mtandao kama facebook?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.