Kampuni mama inayomiliki mtandao unaoenda kwa jina la Tigo, limeshauza bishara zake katika nchi kadhaa Afrika, mtandao wa Tigo sasa ni Tanzania na Chad tuu.
Masoko ya Tanzania na Chad kwa sasa ndio mtandao wa Tigo unafanya vizuri zaidi na kutengeneza mapato kwa kampuni miliki, Millicom.

Nchini Senegal Millicom wapo katika mchakato wa kuuza biashara ya mtandao wa Tigo nchini humo. Kwa Rwanda tayari mtandao huo umenunuliwa na mtandao wa Airtel. Mauzo hayo tayari yameshapewa baraka na serikali ya nchini Rwanda.
Kimapato masoko yanayofanya vizuri ni Tigo Tanzania na Tigo Chad. Katika robo ya mwisho ya mwaka jana masoko haya mawili yalisababisha mapato ya dola milioni 150 za Kimarekani. Na kwa ujumla wake wana wateja 356,000 katika nchi hizo mbili.
Millicom inaonekana katika hatua za kuondoka katika nchi za Afrika na kuzidisha nguvu zake kwa masoko ya bara la Latini Amerika. Mtandao wa ConnectingAfrica unaamini kuna uwezekano Tigo wakauza masoko yote ya Afrika.
Kwa Ghana mtandao huo ulishafanya maamuzi ya kuunganisha biashara zake na za mtandao wa Airtel, hili limeleta shirika jipya la mawasiliano linalokwenda kwa jina la AirtelTigo, na wamepeana umiliki wa asilimia 50 kila mmoja. Kwa pamoja sasa wana watumiaji wa takribani milioni 10 na kulifanya shirika hilo kuwa la pili kwa idadi ya watumiaji.

Kwa Tanzania hatufahamu nini kinaweza tokea, tutaendelea kufuatilia kama kutakuwa na habari yeyote mpya. Endelea kutembelea Teknokona – Kona ya Teknolojia Tanzania.
Chanzo: ConnectingAfrica na mitandao mbalimbali