TikTok, mtandao maarufu wa video fupi, huenda ikajiingiza katika eneo la picha kwa kuja na programu ya kushirikisha(kushare) picha “TikTok Photos” Taarifa za hivi karibuni zinaonesha mtandao huo unamilikiwa na Kampuni kutoka China iitwayo ByteDance upo mbioni kutambulisha progaramu mpaya ambayo itakuwa imekita kwenye picha kama jinsi ilivyo kwa Instagrama Inayomilikiwa na Meta
Hatua hii haishangazi, ikizingatiwa TikTok inampango kwa kujiingiza kwenye soko la programu za kushirikisha picha kwani programu hizo zimekuwa na mafanikio kwenye masoko mbali mbali duniani hata huko China, hususani kwenye miji kama Xiaohongshu, ambayo hutumia mitandao ya kijamii kwenye shughuli za kibiashara mtandaoni. Mapato yanayopatikana na idadi kubwa ya watumiaji ya Xiaohongshu inaonyesha uwepo wa soko kubwa wa mitandao ya kushare picha.
ByteDance, kampuni mama ya TikTok, ina historia ya kujaribu kuzindua programu mpya mbali mbali za kuhariri na kushea picha kama Lemon8, ambayo inalenga biashara mtandaoni pamoja na mitandao ya kijamii. Kuzindua TikTok Photos kunaweza kuwa hatua ya kimkakati ya kujaribu kujingiza kwenye masoko mpya na kujiondoa katika masoko fulani ambapo TikTok inaweza kupigwa marufuku.
Hatua hii si haba, kwani TikTok Photos inaweza kuwa na fursa nzuri, haswa katika masoko ya Magharibi, ikiwa itatekelezwa vizuri.
Kwa kumalizia, uvumi wa TikTok kuingia kwenye picha TikTok Photos unaonyesha azma ya ByteDance ya kupambana na Instagram na kuzidisha mvuto wake wa biashara mtandaoni, ikitoa watumiaji njia mpya za kushiriki na kuunganisha.
No Comment! Be the first one.