TikTok kuendelea kupatikana Marekani kama kawaida baada ya mazungumzo ya awali na Oracle na Walmart kuhusu kuuza sehemu ya biashara yake kwao kuwa ya mafanikio.
App hiyo inayokua kwa kasi tayari ilikuwa katika hatihati ya kufungiwa upatikanaji wake kwenye masoko ya apps nchini Marekani kuanzia Jumapili saa sita usiku. Serikali ya Marekani ilikuwa imeweka siku hii kama ndio mwisho wa upatikanaji huo kama bado app hiyo haitakuwa imeuza sehemu ya kazi zake hasa hasa kwenye eneo la data za watumiaji wa Marekani.
Serikali ya Marekani chini ya Rais Trump kwa muda mrefu wamekuwa hawana imani ya usalama wa app hii inayomilikiwa na kampuni ya Kichina ya ByteDance.
Kwa kuhakikisha data za watumiaji wa Marekani zinakuwa chini ya uangalizi wa kampuni ya Kimarekani serikali hiyo inaamini itakuwa imelinda data za watumiaji wa app hiyo wa nchini Marekani.
Makampuni mengi yalikuwa yanavutiwa na kupata umiliki wa app hiyo maarufu ila inaonekana ni kampuni ya Oracle pamoja na Walmart ndio wameweza kufanikiwa katika mazungumzo na kampuni ya ByteDance.
Inasemakana kampuni ya Oracle itaweza kusimamia shughuli zote za utunzaji data za watumiaji na huku kampuni mpya ya TikTok Global itaundwa huku ByteDance wakibakia na asilimia kubwa ya umiliki na huku asilimia zingine zikienda kwa Oracle na Walmart.
Rais Trump amesema amependezwa na mazungumzo kati ya makampuni hayo na kwamba anaunga mkono makubaliano hayo ambayo tayari yapo hatua za mwisho.
No Comment! Be the first one.