Majukwaa makubwa ya muziki wa ku’stream kwa kawaida yanafanya vizuri na kuingiza mapato mengi kwa makampuni husika, TikTok nao wanataga kipande cha muhogo huo kwa kutangaza mtandao wao yaani TikTok Music.
Kumbuka ndani ya mtandao wa kijamii wa TikTok kuna video nyingi huwa zinaandaliwa kwa kuwekewa na nyimbo juu yake.
Labda kupitia hili mtandao huo umeona ndio moja ya sababu katika kuhakikisha kwamba wanakuja na mtandao wa kwao wenyewe kwa ajili ya maswaka ya muziki wa ku’stream.
Ni wazi kabisa kwamba TikTok ilikuja na ukuaji wa kasi sana, huku namba nyingi ya watu wakiufurahia mtandao huo kwa kasi hali ambayo ilipelekea wengi wao kujiunga.
Ni wazi kwamba TikTok Music pengine inaenda kuleta mapinduzi makubwa sana na kuwa msindani sambamba na mitandao mikubwa kama vile Apple Music n.k
Kwa sasa mtandao huu mpya umeanza kupatikana huko nchini Brazil na Indonesia hii ikiwa kama ni sehemu tuu ya utangulizi wa huduma hiyo mpya ambayo hivi karibuni itamfikia kila mtu.
Kingine ni kwamba TikTok Music itakua inangiliana moja kwa moja na TikTok ya kawaida na hivyo basi wasikilizaji wa muziki wanaweza kusikiliza,ku’share na hata kushusha miziki mbalimbali katika jukwaa hilo.
Hapa utakua na uwezo wa kutumia akaunti yako ya TikTok ili kuendelea kutumia TikTok Music kwa urahisi kabisa.
Kumbuka hili sio jambo jipya kwa TikTok maana mwaka 2020 pia walikuja na mtandao unaoitwa Resso ambao nao ulikua ni wa muziki wa ku’stream.
Kwa ujio huu wa TikTok Music ni wazi kwamba kampuni italazimika kuachana kabisa na mtandao/huduma hiyo ya Resso ambao ulikua unapatika kwa ukubwa kabisa.
Soma Kila Kitu kuhusu TikTok >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je unahisi TikTok Music itakuja kuwa msindani halali kwa mitandao mikubwa kama vile Apple Music Na Spotify?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.