Nchi nyingi duniani hivi sasa uchumi wake umenyuma kutokana na kukumbwa na virusi vya Corona (COVID-19) ambavyo vinavyosababisha homa ya mapafu. Huko Marekani, Bw. Tim Cook amejuishwa kwenye timu ya watalaamu ambao kazi yao ni kuinua uchumi wa California.
Hata kama kuna janga la COVID 19 lakini maisha lazima yaendelee bila kusahau uchumi wa mahali, jimbo na nchi kwa ujumla wake. Ndio, mtendaji mkuu wa Apple, Bw. Tim Cook amejumuishwa na Gavana wa California, Mhe. Gavin Newsom pamoja na watu wegine zaidi ya sabini (70) ambapo kazi yao ni namna gani ya kuinua uchumi wa jimbo hilo ambao umetetereka.
Imekuaje mpaka Mtendaji Mkuu wa Apple kuwekwa kwenye orodha?
Kiongozi huyo mkuu aliyechukua nafasi hiyo baada ya kuachwa wazi na marehemu Steve Jobs ameonekana kuwa anafaa kuwepo kwenye timu hiyo ya wataalamu mahususi kabisa kwa ajili ya kuurudisha juu uchumi wa California kwenye mstari inatokana na mkutano alioufanya na wafanyakazi wake hivi karibuni huku kila mtu akiwa kwake alivyooanisha hali ilivyo hivi sasa na jinsi ya kwenda mbele huku akiongeza kuwa kampuni hiyo ipo vizuri kiuchumi na wataendelea kuwekeza kwenye tafiti na maendeleo ya biashara kwa mapana.
Wataalamu hao kutoka kampuni mbalimbali watakuwa wanakutana mara mbili (2) kwa mwezi kujadili mwenendo wa uchumi ndani ya California na nini cha kufanya kulifanya jiji hilo lirudi katika hali yake.
Chanzo: MacRumors