CEO – Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa sasa wa kampuni kubwa katika masuala ya elektroniki ya Apple, Bwana Tim Cook, inasemekana alitaka kumpatia mmoja wa waanzilishi wa kampuni hiyo, Bwana Steve Jobs eneo la ini lake ili kuweza kunusuru uhai wa Steve Jobs.
Jambo ili limefahamika kupitia kitabu kinachoelezea maisha ya Tim Cook kinachoitwa ‘Becoming Steve Jobs’, yaani kwa kiswahili ‘Kuwa Steve Jobs’ kinachotegemewa kuanza kuuzika hivi karibuni.
Inasemekana Tim Cook alikuwa na mapenzi ya dhati kabisa kwa aliyekuwa bosi wake na mtu aliyekuwa anamkubali sana kikazi, Steve Jobs. Steve Jobs, mtu ambaye anapewa sifa kubwa sana kwa uwezo wake wa kuweza kuleta mabadiliko makubwa katika teknolojia za simu na tableti, na mauzo ya apps, muziki na vitabu kupitia kampuni ya Apple alifariki mwaka 2011 baada ya kusumbuliwa na kansa ya ini kwa muda mrefu.
Soma Pia : Tim Cook wa Apple asema “Najivunia Kuwa Shoga”
Inasemekana kipindi chote cha kuumwa sana kwa Steve Jobs, Tim Cook alijitahidi kuweza kumuona mara kwa mara, na aliumia kila alipokuwa akimkuta katika hali mbaya zaidi. Na pale alipogundua kuwa kama Steve Jobs angepata kufanyiwa oparesheni ya kuwekewa ini jingine ingesaidia kwa sana katika kuboresha afya yake alienda kufanya vipimo kuhusu ini lake yeye na aina ya damu yake. Hii ni kwa sababu ili mtu kuweza kuwekewa ini la mwingine ni lazima mambo mbalimbali yahusuyo masuala ya damu yalingane. Na siyo kwamba ilikuwa inaitajika ini lote bali ni sehemu ndogo tuu ya ini.
Inasemekana baada ya kugundua mahitaji yote muhimu ya yeye kuweza kumsaidia Steve Jobs kwa kufanya oparesheni na kumpatia sehemu ya ini lake Tim Cook alimtembelea Steve Jobs nyumbani kwake na kumueleza jambo hilo. Lakini bila ya kutegemea, Steve Jobs hakukubali, na alimwambia ‘Hapana, sitaweza kukuruhusu ufanye hivyo. Sitaweza kamwe!’
“‘No,’ he said. ‘I’ll never let you do that. I’ll never do that.'” – Tim Cook
‘Steve Jobs amenikaripia kama mara nne au tano hivi kwenye miaka 13 niliyokuwa nafahamiana naye. Na hii ilikuwa ni moja ya hizo siku”, amesema Tim Cook kupitia kitabu hicho.
Mwezi wa tatu, 2009 Steve Jobs alifanya oparesheni ya ini, ila si kwa kutumia ini la Tim Cook.
Kupitia kitabu hicho pia habari ya Steve Jobs kutamani kuinunua kampuni ya Yahoo imeongelewa.
One Comment