Ni kawaida kwa makampuni mengi ya simu kupata malighafi na vipuri kwa makampuni mengine ya pembeni –ndivyo dunia ilivyo—kwa upande wa Apple ni hivyo hivyo.
Japo makampuni mengi kama Apple huwa hayawaweki wazi kila wanapochukua vipuri au malighafi hizo kutokana sababu zao wenyewe, lakini kwa sasa Sony wamewejwa.
iPhone ni moja kati ya simu zenye kamera nzuri zaidi ukilinganisha na simu nyingi ambazo ziko sokoni licha ya kuwa inasifiwa kuwa moja kati ya simu bora sana kuweza kutokea katika uso wa dunia.
Ni kawaida sana kwa kampuni ya Apple kukaa kimya kuwa ni nani anaiwezesha kampuni hiyo katika vitu kama vile Betri, Chipu zake Kioo n.k
Ni hivi karibuni pia iliwashangaza watu baada ya kuweka wazi kuwa kuna baadhi ya vioo vya OLED watakua wakivipata kutoka kwa kampuni ya LG na hii ni ukiachana na Samsung ambayo ndio tulikua tumeizoea na kwa sasa asilimia nyingi ya vioo vya iPhone 14 inatoka kwao.
Iinavyosemekana dili hili kutoka Sony na Apple ni la muda mrefu tuu na vyanzo mbalimbali vinasema kuwa wana mkataba wa muda mrefu na pia wanaanda sense zingine –mpya– kwa ajili ya iPhone.
Taarifa hizi zilitoka ikiwa ni baada ya Tim Cook kuweka picha katika mtandao wa kijamii wa Twitter na picha hiyo ilikua ikionesha akiwa anangalia moja kati ya kamera za iPhone.
“Tumekua tukishirikiana na Sony kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 sasa na tumekua tukijitika katika kuhakikisha tunaleta sensa bora kabisa kwa ajili ya kamera ya iPhone –Picha hiyo kupitia Twtitter iliambatana na maneno haya”
Ukiachana na kutosema vifaa unapata wapi kwa mteja hili sio jambo kabisa sio? Nadhani mteja huwa anataka tuu kupata bidhaa nzuri ambayo haina madhara, maana ni wateja wachache sana watataka kufuatilia kila kitu ili bidhaa ikamilike
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni vifaa gani vingie kampuni ya Apple inapata sehemu nyingine lakini imekaa kimya tuu ukaichana na vile kutoka sony.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.