Historia nyingine imewekwa tena na kampuni ya Nokia, toleo lake la Nokia 6 limefanya maajabu kwani simu zote ambazo zilikuwa stoo ziliuzwa ndani ya dakika moja.
Nokia kwa sasa ipo chini ya kampuni ya HDM Global na liliuza simu za Nokia 6 huko nchini china tuu na ndipo walipopata matunda makubwa.
Mauzo ya simu hii yalifanyika katika mall ya JingDong, aka JD.com, na watu ambao walijiandikisha mwanzoni kabisa kabla hata ya simu haijafika hapo ili ikifika wawe wakwanza kuipata walikua ni zaidi ya milioni moja na laki tatu.
Japokuwa haijulikani kwa undani kuwa Nokia iliuza simu ngapi ndani ya dakika hiyo moja lakini kinachojulikana ni kwamba ziliisha zote ambazo zilikuwa katika stoo. (Kuna taarifa zinazosema inasemekana zilisimu milioni 1).
BEI NA SIFA
- Nokia ilikua inauzika china kwa gharama ya yuan 1699 ambayo ni ni sawa na dola 248 za kimarekani na kwa haraka haraka ni sawa na laki tano za Tz
- Prosesa yake ni entry-level Snapdragon 430 64-bit octa-core ambayo ina Adreno graphic ya 505
- Ram GB 4
- Display ya Inch 5.5 ambayo ni HD (1,920 x 1,080 pixels)
- Ujazo wake wa ndani ni GB 64
- Android 7
Pengine sifa za simu hii ndio zimeipa umaarufu mkubwa ukiachana na kuwa kampuni ya Nokia kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inatengeneza simu ambazo ni imara na zinazodumu kwa muda
Mauzo ya simu hii inasemekana yataendelea tena wiki ijayo ila JD.com bado hawajatangaza siku bado
SIMU ZA NOKIA ZINAZOTUMIA ANDROID
Kitu kizuri ni kwamba kampuni ya HMD Global ina simu kadhaa za Nokia ambazo zinaendesha na Android ambazo zipo katika matengenezo.
Punde tuu simu hizi zitaingia sokoni na inasemekana simu za kwanza kuingia nazo zitakua Nokia 8 na Nokia P1 na hili linategemea kutokea muda wowote ndani ya mwezi wa pili 2017
Japokua Nokia 6 imeuzika China tuu lakini matoleo mengine ya Nokia yanatarajiwa kuuzika katika wigo mpana zaidi (Duniani kote).
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment hii umeipokea vipi?
One Comment
Comments are closed.