Kama unapenda kuangalia muvi basi endelea kusoma makala hii uweze kufahamu tovuti za kupakua muvi mtandaoni. Kuna tovuti nyingi za kupakulia muvi na tamthilia mtandaoni lakini hizi ndo maarufu zaidi.
Yts: Hii ni tovuti maalum kwaajili ya kupakulia muvi zenye ubora wa hali ya juu (HD). Unapoingia katika tovuti hii utakutana na orodha ya muvi mpya zilizotoka lakini pia utaweza kutafuta muvi za zamani katika sehemu ya kutafuta na kuipakua. Pia unaweza kuangalia trela ya muvi kabla haujaipakua na kusoma maelezo mafupi kuhusu maudhui ya muvi hiyo pamoja na waigizaji waliopo katika muvi hiyo.

Piratebay: Tovuti hii ni maarufu sana, unaweza kupakua mambo mbalimbali ndani ya tovuti hii kama muvi, tamthilia, gemu, programu za kwenye kompyuta, vitabu na mambo mengine mengi. Hautaweza kuona picha wala kupata maelezo yoyote ya ziada kuhusu kitu unachokipakua unapokuwa kwenye tovuti hii. Unashauriwa kuchukua tahadhari dhidi ya wadukuzi unapotembelea na kupakua mafaili katika tovuti hii.
13337x: Tovuti hii pia huwa na mambo mengi kama muvi, tamthilia pamoja na programu za kompyuta. Unapotaka kupakua muvi katika tovuti hii unatakiwa kuitafuta kwanza katika sehemu ya kutafutia halafu ukiiona utaibonyeza na kupelekwa katika kurasa ya kupakulia hiyo muvi. Hautaweza kuona picha yoyote wala maelezo ya ziada kuhusu hiyo muvi unayotaka kupakua.
Kissasians: Tovuti hii ni maalum kwaajili ya muvi na tamthilia za kikorea na kichina. Unapotembelea tovuti hii utaweza kuona muvi na tamthilia mpya za kichina na kikorea lakini pia unaweza kutafuta muvi hizo kupitia sehemu ya kutafutia. Tovuti hii inaruhusu kuangalia moja kwa moja mtandaoni na pia kuipakua hiyo muvi au tamthilia unayoitaka.
O2tvseries: Hii ni tovuti maalum kwaajili ya kupakua tamthilia mbalimbali nyingi zikiwa ni za marekani. Unapotembelea tovuti hii utaona orodha ya tamthilia zote zilizopo kwenye tovuti hiyo na utaweza kujichagulia ni tamthilia ipi ungependa kuipakua. Sifa kubwa ya tovuti hii ni kwamba unaweza kupakua na kuangalia tamthilia kupitia simu janja yako.

Endelea kutembelea tovuti yetu uweze kujifunza mambo mbalimbali kuhusu teknolojia na pia kupata uelewa zaidi wa matumizi sahihi ya huduma za mtandaoni. Soma makala zetu nyingine hapa.
No Comment! Be the first one.