Tanzania Telecommunications Company (TTCL) ina mpango wa kukodisha muunganisho wa intaneti kwa Uganda, ambayo inataka kujenga mbadala kutoka kutegemea muunganisho kupitia Kenya hapo Novemba, (Daily News).
Hatua hiyo itawafaidisha watumiaji wa intaneti na kuwa kama ulinzi dhidi ya utegemezi wa cable moja (kupitia Kenya), na kuboresha kasi, na upatikanaji wa kuaminika wa intaneti nchini humo.
Afisa wa TTCL Nikodemo Mngulu aliiambia gazeti la DailyNews kuwa ujenzi wa cable mbadala bahari utategemea kiasi gani cha Bandwidth Uganda itakuwa inatumia. Uganda itakuwa inalipia kutumia cable kutoka Dar es Salaam hadi Mtukula(Kagera) kwenye mpaka wa kuingia Uganda.
Nchini Uganda, matumizi ya intaneti yameendelea kukua mno ambapo watumiaji wamefikia milioni tano mapema mwaka huu. Hata hivyo, huduma hiyo imeendelea kuwa isiyo ya uhakika kutokana na kutegemea cable moja inayoingia kupitia Kenya, kunapotokea itilafu yeyote upande wa Kenya watu binafsi na biashara nyingi zinaathirika na kulazimika kutumia mfumo ghali wa
Nawaombea mafanikio katika dili hili, ufisadi tuu ukae mbali na mambo yaende fresh TTCL wafanikiwe.
No Comment! Be the first one.