Shirika la Teknolojia ya Mawasiliano la Japan, NEC, limeingia katika mkataba wenye thamani wa dola milioni 1.6 za Marekani (Tsh 2,660,800,000/=) ili kuboresha uwezo wa mfumo wa mawasiliano ya simu kwa zaidi ya mara mbili ya uliopo sasa, hii ni pamoja na kukuza kasi ya huduma ya intaneti.
Waziri Makame Mbarawa amesema uboreshwaji huo (ugrades) ni muhimu katika kusaidia taifa katika kufanikisha mpango wa taifa wa 2025 (Vision 2025), hii ni katika katika kuhakikisha kitengo cha mawasiliano kisaidie ukuaji wa nyanja zingine za kiuchumi.
Teknokona tunasubiri kuona kama hatua hii itasaidia katika kulifanya shirika hili liweze kushindani vizuri na makampuni mengine. Kwani ni hakika TTCL wapo katika nafasi nzuri sana ya kukuza utumiaji wa huduma za intaneti za waya (broadband) na Faiba (fiber). Wao ndio wanasimamia teknolojia kubwa zaidi za mawasiliano Tanzania.
Kwa taarifa za mwaka 2013 ni asilimia 14 tuu ya watu Tanzania wanahuduma za intaneti ya nyumbani (fixed internet), na ni asilimia 0.4% tuu ndio wanamiliki simu za mezani.
TTCL wanauhusiano wa kupewa huduma za kiteknolojia na shirika la NEC tokea mwaka 1972, na ni shirika lenye ujuzi wa zaidi ya miaka 100 katika masuala ya teknolojia ya mawasiliano (ICT).
No Comment! Be the first one.