Jana tuliripoti kuhusu taarifa za udukuzi uliodaiwa kufanywa na kundi la kiharakati za kimtandao la ‘The Anonymous’. TTCL baada ya kuchunguza data hizo wamesema jambo ilo halijafanyika kama linavyodaiwa.
Ila kinachoonekana kuwa ni cha kweli ni baadhi ya taarifa zilizo kwenye data hizo, ila inaonekana taarifa za wafanyakazi zilizokuwepo ni za wafanyakazi wasio kwenye shirika ilo kwa sasa.
Wengi wao walishastaafu, kuondoka na ata kufariki. Ingawa data hizo ni za watu 64,000 shirika hilo kwa sasa lina wafanyakazi 1,557 tuu nchini kote.
Uhakikishaji huu kutoka TTCL unaonesha ya kwamba labda kundi hilo lilifanikiwa kufikia data zisizokuwa za umuhimu wowote kwenye mfumo wa tovuti ya TTCL na si kwenye mitambo data muhimu ya shirika hilo kama walivyodai.
Vyanzo: DailyNews na vinginevyo
No Comment! Be the first one.