Licha ya App hii kukua kwa kasi ndani ya kipindi cha mda mchache bado haijatosheka na ukuaji huo. App ya snapchat bado inaendelea kufanya maboresho na vipengele kadha wa kadha. Kumbuka hapo awali App hiyo (SnapChat) iliongeza ‘Filter’ mbali mbali kama lenzi na zingine.
Yote haya yanafanyika kwa lengo la kuwavutia watumiaji wapya katika App hii na hata wale watangazaji. Ili kufanya hivyo Snapchat imeingiza vipengele vingine katika App Yake. Vipengele hivyo ikiwa ni kama hatua ya App kukua kimaboresho zaidi.

Maboresho au vipengele vipya vilivyoongezwa ni vya aina tatu katika video yaani; fast-forward, slow Motion na rewind ikiwa na maana ya Kusogeza mbele kwa kasi, Kupunguza kasi na Kurudisha nyuma. Vipengele hivi vitatu vitaonekana katika Snap za video tuu na sio zile za picha

Fast Forward: Hii inafanya video kucheza katika spidi ya kasi sana na ni nzuri kwa wale wanotengeneza video zenye ‘effects’ au hata comic
Slow Motion: Hii inapunguza kasi ya video na kumfanya mtazamaji aone vitu vingi ambavyo pengine asingeviona kama ingekuwa inacheza kawaida.
Rewind: Hii inakuwezesha kuangalia video kwenye kasi ile ile ila kwa kinyume yaani kutoka mbele kurudi nyuma

Ukiachana na vipengele hivyo vipya vitatu katika video pia snapchat imeleta maboresho na haya yamejikita kwa watumiaji wa iOs kutokana na kuingia kwa iPhone mpya sokoni na programu endeshaji mpya ya simu za iOs.
Uwezo Wa Tachi Ya 3D
Hili sio la kushangaza sana kwani hata hapo awali wakati tunafanya tathimini ya simu za Apple zile za iPhone 6s na 6s Plus tulieleza kuhusu kipengele hiki

Katika simu hizo simu itachagua ifanye kitu gani kutokana na jinsi unavyobofya kioo cha simu yake ya iPhone. Jinsi ya kutumia kipengele hiki mtumiaji wa snapchat katika iOs itambidi abofye App hiyo kwa nguvu ili achague kama anataka kuongeza rafiki (Add a friend) au kama anataka kuchati na rafiki (Chat a friend).
Mengi tumeona katika mtandao huu wa snapchat na hata hviyo inaonekana dhahiri kuwa App hii inapigana katika kuwa App namba moja na kuzipita zile nguli kama vile WhatsApp na Instagram. Tuliona pia Snapchat ikiongeza kipengele kile cha kulipia ili kuangalia tena kama hukuona snap vizuri
One Comment