Apple ni moja kati ya makampuni makubwa sana katika Nyanja ya sayansi na teknolojia. Mara kwa mara kampuni imekua ikija na vifaa ambavyo vinaleta mapinduzi makubwa katika teknolojia na sasa ni zamu ya Vision Pro.
Ikumbukwe Apple ndio wamiliki wa vifaa kama vile iPhone, iPad, Mac na huduma zingine nyingi tuu kama vile uhifadhi wa mtandaoni (Cloud services), Siri na kadhalika. Sasa kampuni imeamua kuja na Vision Pro.
Najua mpaka sasa bado utakua unajiuliza Vision Pro ni nini? Jibu ni hili hapa.
Vision Pro ni kifaa cha AR (Augmented Reality) kutoka Apple ambacho unakifaa katika macho na pengine hiki ndio kinaweza kuwa kifaa ambacho kina ubunifu mkubwa kutoka Apple tangia kuachiwa kwa iPhone.
Teknoljia ya Augmented Reality ina uwezo wa kuonesha vitu –vingine— katika mazingira ambayo ni halisia kwa kutumia kifaa kwenye macho au kwa kutumia kamera ya kifaa kama vile simu n.k.
Kwa haraka haraka ni kwamba kifaa hiki kina sensa na kamera nyingi sana na unakivaa usoni –hakifuniki uso wote—na kingine ni kwamba hutaweza kuunganisha kifaa hiki na iPhone au Mac maana kinakua kinajitegemea.
- Kifaa hiki kitaanza kupatikana mwakani na kitauzika kwa gharama ya dola za kimarekani 3,499(Zaidi ya Tsh milioni 8.2) na kitakua na uwezo wa kukaa na chaji masaa mawili (ukiwa unatumia).
- Kifaa hiki kinajitegemea kwa kiasi kikubwa sana ni kama kompyuta inayojitegemea tuu maana ina WiFi yake, ina chip ya M2, kioo chake ni cha 4K na kinatumia teknolojia ya Micro-OLED na pia ina spika katika kila sikio.
Uzuri wa Vision Pro ni kwamba itakua na uwezo wa kuona nini kipo katika mazingira yayokuzunguka n.k.. mfano kama uko sebuleni itakua na uwezo wa kuona kila kitu kama jinsi jicho lako linavyoona tuu.
Kifaa hiki kitakua hakuna kitu ambacho kinatumika kukiendeshea kama vile remote….. hapa utakiendesha kwa kutumia mikono yako, sauti yako na kwa kutumia macho yako –kumbuka kinafunika mpaka machoni.
Mpaka sasa kifaa hiki kinakuja na Apps za Apple tuu (japokua bado hakijaachiwa—pengine mbeleni wataweza kuongeza baadha ya Apps
Kwa sasa ni App Hizi: Apple TV, Apple Music, Settings, App Store, Safari, Photos, Memos, Messages, Mail
Na kadhalika –kutoka Apple tuu
Apple wamesema kwamba Vision Pro itaingia sokoni mwakani pengine ni kuwapa waandaaji wa App kutengeneza App zao ili kuendana na mfumo huo ili App zao zianze kupatikana humo. Ila tayari wamesema kuna apps nyingine nyingi ambazo tayari zinafanyiwa kazi na zitaanza kufanya kazi kwa ubora mkubwa kwa watumiaji wa Vision Pro.
Kingine cha kuwekea maanani ni kwamba kifaa hiki ni kipya kabisa na kinajitegemea hata program endeshaji ni mpya na imepewa jina la Vision OS.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment je unaweza ukaanza kutumia kifaa hiki kikianza kupatikana katika soko?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.